Ushauri kwa mwanaume wa miaka 35

Habari zenu Thinkers.

Kwa mwanaume aliefikia miaka 35. Je Ushauri gani unaweza mpatia.

Kuwa free kwenye maeneo yote ya Maisha. Afya, Uchumi, Social, Spiritual.

Karibuni sana.
Angalia maisha yako.

Sio kila mwanamke unaempenda umtokee,wengine unawapenda potezea utawasahau,itakuepusha na gharama zisizo na msingi.

Hakikisha una shughuli ya kujiajiri hata kama umeajiriwa.

Hakikisha unakuwa mtu asiyeongea pumba ukiwa na watu haijalishi umri wao.

Hakikisha unaweza kucontrol nyege zako kwa namna yeyote ile mradi usijivunjie heshima
 

Umenena vyema sana. Hii post ndio imenikumbusha mwakani I'm turning 35
 
Nashukuru Sana.
 
Nashukuru sana.
 
1. Oa
2. Wekeza hata kwa kiasi kidogo
3. Jitume kwenye kila kazi ufanyayo
4. Acha anasa
5. Starehe kiasi
6. Kuwa na marafiki wenye faida/maana
7. Kuwa na marafiki wakubwa kwako kiumri
8. Fanya ibada
9. Heshimu na linda familia yako
10. Kuwa na msimamo binafsi usiwe muoga
 
Nashukuru sana Mgeni, elimu nzuri sana hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…