Ushauri kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa. Jikite katika kukitangaza chama na kumtangaza mwenyekiti

Ushauri kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa. Jikite katika kukitangaza chama na kumtangaza mwenyekiti

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Habari,

Heri ya sikukuu ya Noeli kwa wakristo wote. Leo ni siku nyingine tumesheherekea kuzaliwa kwa mwokozi wa ulimwengu kwa hiyo ,pamoja na wakristo wengine tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa pamoja nasi na kwa zawadi hii kubwa.

Kabla sijaenda kwenye mada husika ningependa kuuliza maswali haya mawili kwa mwenyekiti wetu wa UVCCM Taifa:

i) Je, upo kwenye nafasi hiyo kwa maslahi ya chama au binafsi?

ii) Kwa nini unatumia nguvu kubwa kujieneza badala ya kueneza chama?

Kwanza kabisa, naomba ku-declare kwamba sina chuki binafsi na Ndg.Kawaida na zaidi namheshimu kwa nafasi yake ya uongozi. Nafasi yake ni kubwa na ya heshima kubwa na ambayo inaweza kuunganisha vijana wengi zaidi na kutengeneza mazingira mazuri kwa Mwenyekiti wa CCM kukubalika.

Kwa siku hizi chache toka kuchaguliwa kwako kuna Mambo nayaona sio ya kawaida ndg.Kawaida.

Kwanza, Ndg.Kawaida nimeona mitandaoni kuna 'team' zimeundwa na ninaamini zimeundwa na watu wa IT wa UVCCM. Mojawapo ya Team hiyo ni "Teamkawaida". Baada ya kuziona team hizi zinazoku-promote sana badala ya kukipromote chama nilishangaa na kushtuka sana.

Kimsingi, Viongozi na wanachama wote wa UVCCM kazi yao ni kukisaidia Chama na kumsaidia Mwenyekiti, sasa "Team Kawaida" ipo kwa lengo gani?

Kama baada ya uchaguzi kuisha team zote zinavunjwa ,je teamkawaida Ina umuhimu gani baada ya uchaguzi?

Pia ,kuna kitu nakiona kwa Ndg.Kawaida, katika mwendelezo huohuo wa kujipromote naona hadi T-shirt anazovaa zina nembo ya jina lake? Sijajua nembo ya T-shirt na sare za chama zinatakiwa ziwe na nembo tofauti au picha tofauti na ya Mwenyekiti wa Chama, sasa kwa nini Kawaida anavaa sare zinazompromote?

Naomba nitoe ushauri mdogo kwako Ndg.Kawaida jikite katika kukiineza chama na uache kutafuta umaarufu binafsi na pia utambue dhamana ya Chama ipo chini ya Mwenyekiti wake Taifa Ndg.Dkt.Samia Suluhu hivyo usitumie majukwaa uliyonayo kujipromote na badala ya mpromote Mwenyekiti wa CCM.

Naamini wewe ni msikivu na ushauri huu utauzingatia na kuutekeleza. Ukitaka ushauri zaidi wa athari zitakazotokana kwa kutofuata ushauri huu kwa CCM nitafute kwa namba 0685655580.
 
Habari,

Heri ya sikukuu ya Noeli kwa wakristo wote. Leo ni siku nyingine tumesheherekea kuzaliwa kwa mwokozi wa ulimwengu kwa hiyo ,pamoja na wakristo wengine tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa pamoja nasi na kwa zawadi hii kubwa.

nitafute kwa namba 0685655580.
Mkuu Isakashe..., umetoa ushauri mzuri.
Merry Christmas.
P
 
Yaani aache kujitangaza kwani CCM inalindwa na wanachama au vyombo vya dola? Sasa kama unataka ampromote mwenyekiti, kwani mwenyekiti ndio chama? Kazi ya kuilinda CCM kisiasa wanachama walishashindwa.

Hivyo vyombo vya dola ndio kinga yao kwa ushirikiano wa vijana wahalifu walio ndani ya CCM, ili waachiwe wafanye shughuli zao haramu.
 
Yaani aache kujitangaza kwani CCM inalindwa na wanachama au vyombo vya dola? Sasa kama unataka ampromote mwenyekiti, kwani mwenyekiti ndio chama? Kazi ya kuilinda CCM kisiasa wanachama walishashindwa, hivyo vyombo vya dola ndio kinga yao kwa ushirikiano wa vijana wahalifu walio ndani ya CCM, ili waachiwe wafanye shughuli zao haramu.
Anatakiwa kumpromote Mwenyekiti kwa sababu Mwenyekiti ndio mwenye dhamana yote ya Chama kwa niaba ya Chama

CCM ni mali ya wanachama na maslahi yake hayana budi kulindwa na wanachama.

Sio kweli kwamba wanachama wameshindwa kukilinda chama, Ingekuwa hivyo wanaCCM wasingekuwa na furaha lakini wanaCCM ndio wanaongoza kuwa na furaha na Chama chao.
 
Anatakiwa kumpromote Mwenyekiti kwa sababu Mwenyekiti ndio mwenye dhamana yote ya Chama kwa niaba ya Chama

CCM ni mali ya wanachama na maslahi yake hayana budi kulindwa na wanachama.

Sio kweli kwamba wanachama wameshindwa kukilinda chama, Ingekuwa hivyo wanaCCM wasingekuwa na furaha lakini wanaCCM ndio wanaongoza kuwa na furaha na Chama chao.

Wañaccm wataacha kuwa na raha, wakati wanapata ulinzi wa vyombo vya ili waile vizuri cake ya taifa? Hata bila kumpromote, tayari kofia ya urais inampromote mwenyekiti wa CCM. Hivyo hakuna ulazima wowote wa yeye kumpa promo.

CCM ni mali ya wanachama kwa sababu za kihistoria, lakini kiuhalisia ni chama cha wajanja wachache wanaokula kwa ulaini. Wañaccm wangekuwa na uwezo wa kukilinda, tusingeona vyombo vya dola vikiacha kufanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria, na badala yake kugeuka walinzi wa chama cha wezi.
 
Back
Top Bottom