Ushauri Kwa Ndugu Mchengerwa (Mbunge)waziri wa Utumishi

Ushauri Kwa Ndugu Mchengerwa (Mbunge)waziri wa Utumishi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Habari Mhe Waziri , Mohammed Mchengerwa ,Kwanza ni kupongeze Kwa uteuzi wako ,kazi unaenda nayo vizuri ,kuna maeneo kidogo ningependa kushauri ,JF ni kioo cha jamii kitumie katika kujirekebisha.

Ni ukweli usiopingika umekua mtetezi wa Watumishi wa UMMA ukitamani kila mtumishi apate haki yake ,na wasimamiz wao wasiwaonee Kwa ilo nakupongeza sana.

Umekua ukitoa matamko mbalimbali ya kuwakumbusha viongozi wetu ,na watumishi na mengine ukikemea ubabe Kwa Watumishi

Kuna siku ulikemea kutaka viongozi wasituambue watu majukwaani ,tena umekemea viongozi wanatumia ubabe kuwanyima likizo watumishi ukiwataka kufuata sheria na kanuni Kwa maelewano ,ni Jambo jema na matumaini Kwa watumishi

Ila nimeshangaa juzi na wewe umemtumbua afsa manunuzi wa TARURA jukwaani ,nimetaka nikuweke Sawa usimamie unachowakumbusha wenzako ,naamini utalipokea na kulifanyia kazi.

NB: Serikali iongeze mwendo katika kulipa madeni ya wafanyakazi, ulipoteuliwa ulitangaza kuwa serikali imetenga fedha za ulipaji wa madeni na Rais siku ya wafanyakazi Alisema mwaka huu wa fedha utatumika kulipa madeni ya watumishi, mwendo tunaona ni mdogo
 
Habari Mhe Waziri , Mohammed Mchengerwa ,Kwanza ni kupongeze Kwa uteuzi wako ,kazi unaenda nayo vizuri ,kuna maeneo kidogo ningependa kushauri ,JF ni kioo cha jamii kitumie katika kujirekebisha...
Ubarikiwe.
 
Habari Mhe Waziri , Mohammed Mchengerwa ,Kwanza ni kupongeze Kwa uteuzi wako ,kazi unaenda nayo vizuri ,kuna maeneo kidogo ningependa kushauri ,JF ni kioo cha jamii kitumie katika kujirekebisha...
Hivi alitumbua au alielekeza kutumbua. Kwanza hilo neno kutumbua nadhani limeondoka. Mh Waziri aliagiza mtu kusimamishwa na mamlaka ili uchunguzi ufanyike.

Niungane na wewe kumpongeza Mchengerwa kwa jinsi anavyopambana na kupambania watumishi. Naona ni Waziri pekee ambaye anapambana na kuipigania serikali; ingekuwa wakati ule wa Hayati Mkapa basi huyu angekuwa Waziri wa Mwamvuli.
 
Habari Mhe Waziri , Mohammed Mchengerwa ,Kwanza ni kupongeze Kwa uteuzi wako ,kazi unaenda nayo vizuri ,kuna maeneo kidogo ningependa kushauri ,JF ni kioo cha jamii kitumie katika kujirekebisha...
Nadhani umemisi point moja, huyo afisa hajatumbuliwa kama unvyosema bali amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma ambazo Waziri amepewa au ameziona hivyo anapisha uchunguzi na itakaa Kamati ya Mamlaka yake imsikilize ikiwemo kupokea ushahidi na ikijiridhisha kwamba ametenda hayo makosa basi taratibu za kumfukuza kazi ndio zitafuata.
 
Wakuu wa idara kwenye ofisi nyingi wanatoa night kwa upendeleo wamulikwe..maafisa utumishi wakija wafanyakazi wanaogopa kusema...
 
Hivi alitumbua au alielekeza kutumbua. Kwanza hilo neno kutumbua nadhani limeondoka. Mh Waziri aliagiza mtu kusimamishwa na mamlaka ili uchunguzi ufanyike...
Kusema ukweli waziri huyu yupo vizuri sana...Mungu amlinde dhidi ya mahasidi!
 
Yaani nampenda sana Mchengerwa, he matches with the position he holds. Hongera sana, angalau anaonekana kuimudu nafasi ya Captain Mkuchika vilivyo.

Yaani jamaa anachapakazi mpaka uhusiano wake na Hangaya hauzungumzwi. Hajikwezi kabisa..

Hivi huyu kwa jina la kificho ndiye WAZIRI WA USALAMA WA TAIFA?
 
Ndio boss wao huyo kiwizara
 
Back
Top Bottom