Ushauri kwa R.E.O wa Lindi

Ushauri kwa R.E.O wa Lindi

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
We kiongozi unaweza! Hilo ndo pekee lililopo la kusema kuhusu wewe!!!

Naomba nijaribu kushauri yafuatayo;

1. Sherehe za utoaji wa zawadi mwaka huu (kama zipo) hazitokuwa za haki kama walimu walioingiza masoko yao katika kumi bora ya ufaulu (kidato cha nne) ya mkoa hawatozawadiwa......hata ukichukua 3 wa mwanzo poa tu lkn linastahili zawadi kundi hilo, kwa kila somo.

Pia nashauri kuwe na ģzawadi kwa mwenye/wenye asilimia kubwa ya ufaulu kwa daraja I‐III au aliyeongeza ufaulu wa madaraja hayo. Hii inatokana na ukweli kuwa daraja la nne sasa, kitokana na ushindani wa kielimu, ni sawasawa na kufeli tu. Nilishuhudia shule moja ikipata zawadi kwa ufaulu wa 100%, lakini ufaulu wenyewe ni kuwa watoto walikuwa 5 na wote walipata daraja la nne na shule ilikuwa ina walimu sita. Hiki ni kichekesho (speaking the truth). Tena ikiwezekana kigezo cha ufaulu wa 100% kitolewe na kuwekwa hiki.

Toa zawadi kwa shule ambayo/ambazo zimefanikiwa kumaintain upatikanaji wa daraja la I. Namaanisha kuna shule zilikuwa hazina h8storia ya kupata xaraja la kwanza lkn kwa sasa zinapatikana, tena zingine miaka mitatu au zaidi idadi ya I haishuki; wanastahili recognition hawa hata kama ni makofi tu.

2. Angalia/fuatilia vizuri hili suala la mitihani......hawana muda wa kupumzika wala kufanya uchambuzi yakini wa maswali walimu wako kwa ajili ya wanafunzi wao.

January mwishoni test na kusahihisha,

February kuanza kuandika upya maandalio yanayoendana na kalenda iliyotolewa.......na marufuku kuchapa, andika kwa mkono hata km una masomo saba. Wengi wana masomo zaidi ya manne. Feb hiyohiyo kutunga mitihani miwili miwili (monthly na mock zikiwa na marking schemes zake.....hii ni ngazi ya wilaya/halmashauri sasa maana nao wana mipango yao). Mazoezi, remedial, homeworks, usimamizi wa prepo na utoaji na ukaguzi wa notes nao inabidi waufanye kila siku huku weekly test wakilazimika kuzitunga na kuzisimamia kila jumamosi......hakuna kwenda shamba wala kufanya ujasiriamali mwingine.

Juu ya hayo yote, tayari mwezi machi kuna mitihani tena. Kiongozi, walimu hawa wamefundisha muda gani?!!!!!! Watamaliza muda gani mada zenyewe?!!!!!!!! Utakuja kuhukumu watu kwa uonevu! Litafakari kwa kina hilo (ikikupendeza).

3. Wale watoto wanaosoma Mitwero sekondari na kuishi vijiji vya katikati yaani kikwetu, masasi ya leo, likong'o, mtomkavu n.k tafadhali tumia mamlaka na ushawishi wako kumaliza lile tatizo. Kuna hatari kuubaa mno pale. Jioni hadi usiku wa saa mbili hadi nne wanaonekana tu mabarabarani wakitembea kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri. Huwa wanasimamisha na kuomba lifti gari lolote tu wanalokutana nalo......hii ni hatari mno kutokana na hali halisi ya dunia kwa sasa ambapo hadi biashara ya viungo vya binadamu ipo. Tafadhali sana.

Ngoja niishie hapa kwa leo!

Nb: kuna mtaaluma yuko manispaa pale, asipobuni na kutuma template za kujaza angalau mbili kwa siku anaumwa! Tena kuumwa kwenyewe anaweza akalazwa kabisa!
 
Huyu afisa elimu mkoa wa lindi nasikia ndio wanamtumia kama "shamba darasa" wengine wanajifunza kupitia kwake..nini siri ya pazia mkuu?
 
Back
Top Bottom