Ushauri kwa Rais Samia kuhusu zao la Korosho msimu wa 2021

Ushauri kwa Rais Samia kuhusu zao la Korosho msimu wa 2021

Joined
Jun 21, 2021
Posts
32
Reaction score
29
Ndugu wanabodi wenzangu,

Nimesukumwa na nia ya dhati ya kutoa ushauri wa namna tunavyoweza kunusuru anguko baya la bei ya zao la korosho kwa msimu wa 2021 unaotegemea kuanza mnamo mwezi Oktoba 2021.

Korosho ni zao linauzwa nje (export crop) kwa miaka yote na hivyo huchangia katika uingizaji wa pesa za kigeni, lakini pia nchi hufaidika na export levy kwa korosho ghafi.

Kutokana na athari za janga la Corona, viwanda vingi vya kusafisha korosho vilivyo mashariki ya mbali bado vimefungwa, lakini pia usafiri wa majini umepanda maradufu na licha ya kupanda hata kupata ratiba ya kusafirisha mzigo kwenye meli bado ni ngumu. Nimemsikia Balozi wa Tanzania nchini China akizungumzia gharama kupanda kwa container ya futi 20 toka usd 1500 hadi usd 1000.

Upandaji huu ni mkubwa na bila shaka yoyote utaongeza gharama kwa mnunuzi na yeye kulazimika kuweka gharama hizo muuzaji na hii itapelekea bei kushuka sana. Mathalani wastani wa bei kwa mwaka uliopita ilikuwa shillingi 2500 kwa kilo, hivyo kama usafiri umepanda kwa asilimia zaidi ya 600 na bei itaanguka zaidi.

Nini kifanyike, ushauri wangu ni azma ya dhati ifanyike hii korosho iliwe na watanzania wa ndani. Hii ikimaanisha wauzaji wakubali kuweka bei za kizalendo. Kwa mfano kilo moja korosho iliyobanguliwa hupatikana kutoka kwenye kilo nne hadi tano zilizo na maganda, hivyo kama bei ya sokoni itakuwa shs 2000, hivyo korosho safi iuzwe kati ya shs 9000-1000 kwa kilo.

Taarifa za upatikanaji pia zielezwe korosho hii itauzwa katika maduka yepi ili kusiwe na tatizo la upatikanaji.

Tukifanya hivyo wakulima wetu watapata uhakika wa malipo kwa wepesi japo yanaweza kuwa chini ya matarajio yao. Naamini hili linawezekana, tuunge mkono vya kwetu.
 
We ni mgeni sana kwenye hii industry?

Kwanini bei ya korosho ianguke wakati Ufuta na Mbaazi bei ni nzuri sana kwa mwaka huu?

Ufuta mwaka jana bei ya juu ilikuwa 2100 mwaka huu imefika mpaka 2600. Mbaazi zilikuwa 800 mwaka huu zimefika 1500 na bei inaendelea kupanda. Na zote hizi zinasafirishwa kwenda huko nje.

Huko India wakati Covid inawapiga mwanzoni mwa mwaka huu ulikuwa msimu wa korosho West Africa na bado walinunua kwa bei nzuri, kwanini sasahivi wanunue kwa bei ya chini wakati tayari ile wave ilishapita?
 
Halafu tuna uwezo wa kubangua Tani Laki mbili za korosho au unajiandikia tu hapa? Uwezo huo tungekuwa nao ile iliyonunuliwa na serikali tungeibangua wenyewe. Ila iliishia kukaa ghalani mwaka mzima
 
Tuliambiwa kuwa watanzania tutagawiwa korosho tuzitafune tuboreshe afya ya uzazi na mzee wetu wa mtazibangua kwa meno.
 
Back
Top Bottom