Napenda kumshauri Mh. Rais kama atafanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri siku za usoni kufanya yafuatayo:
1. kupunguza ukubwa wa serikali yake kwa kuwa na wizara zifuatazo. wizara ya Elimu, Afya, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama wa raia, Sheria, Habari na mawasiliano, Kilimo na Ushirika, Uchukuzi na usafirishaji, Fedha, Ujenzi, Michezo na Utamaduni, Viwanda na Biashara, Nishati na Madini, Mipango na Uwekezaji, Ardhi na Makazi, Utawala bora na Tathimini. Kazi na Utumishi, Maji na Mazingira.Jumla wizara kumi na nane tu.
2. Kila wizara iwe na Naibu waziri mmoja tu.
3. Halmashauri za wilaya ziwajibike moja kwa moja kwa Wizara husika kupitia idara zilizopo ngazi ya Halmashauri.
4. Ondoa nafasi za mawaziri wa nchi katika ofisi za Rais, Makamu na Waziri Mkuu.
5. Waziri Mkuu apigiwe kura na Wabunge baada ya mapendekezo yako ya majina mawili.
Pia wana Jf mnaweza kutoa mchango wenu wa namna ya kupunguza ukubwa wa serikali ili kuboresha uwajibikaji wa serikali kwa wananchi.