Ushauri kwa Serikali: Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mali zake ziuzwe na zigawanywe kwa walimu kisha chama hiki kifutwe

Ushauri kwa Serikali: Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mali zake ziuzwe na zigawanywe kwa walimu kisha chama hiki kifutwe

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
CWT hakuna msaada wowote kwa mwalimu zaidi ya kumkata kuanzia shilingi elf 15,000 hadi elf 60,000 kwa mwezi kulingana na daraja lake, kisha hizo pesa zinaliwa na wajanja wachache.

Kupitia hizo pesa, chama kimeweza kutengeneza miradi mbalimbali na hadi kufungua bank (MCB) kwa fedha hizi hizi za walimu, na hakuna mwalimu anapata faida hata mia, ila wajanja wachache! Hakuna mwalimu anajua mapato na matumizi ya kila mwezi isipokuwa wajanja wachache tu!

Kwanini chama hiki kisifutwe kisha mali zitaifishwe na kila mwalimu apewe angalau kifuta jasho kufidia machungu?
 
Naunga mkono hoja,na Kwa kuongezea iundwe tume ya uchunguzi kuwachunguza viongozi wote wa CWT waliopita na waliopo wakibainika na kashfa ya ufujaji mali/ubadhilifu wafunguliwe kesi mahakamani.
 
Mpwayungu Village! Vp aisee hii mada hadi sasa hujatoa yako ya moyoni ukiwa ni mdau namba 1 wa taaluma ya ualimu humu jf! Mkuu bila mchango wako wana jf tutaandamana hadi ofisi za jf mikocheni na tukitoka hapo makao makuu ya CWT Ilala! Tunakusubiria!
 
Tuuze CCM kwanza na mali zote tugawane watanzania na wadanganyika wote
 
Ck Allan ! Wewe ukiwa kama mdau una haki ya kuliwasilisha hili mahakamani! Humu Jf utapata tuu maoni lakini hakuna action yoyote inaweza fanya humu, May be wasiliana na Mpwayungu Village ambaye ni mdau mkuu wa taaluma ya Ualimu kwenye Social Media Tanzania! Ila kwa sasa nadhani yupo Dodoma Bungeni kufuatitila Bajeti ya MoF
 
Hilo ni tawi la sisiemu, system inanufaika sana na hiki chama cha wajinga, hivyo ni ngumu kukifuta.
 
Ck Allan ! Wewe ukiwa kama mdau una haki ya kuliwasilisha hili mahakamani! Humu Jf utapata tuu maoni lakini hakuna action yoyote inaweza fanya humu, May be wasiliana na Mpwayungu Village ambaye ni mdau mkuu wa taaluma ya Ualimu kwenye Social Media Tanzania! Ila kwa sasa nadhani yupo Dodoma Bungeni kufuatitila Bajeti ya MoF
Tatizo kupata wanasheria watakaosimama nawe katika jambo hili..
 
Back
Top Bottom