Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Kwa wote wanaohusika,
Awali napenda kuipongeza Serikali kwa kuja na wazo la maombi ya kazi za Sensa kufanyika ONLINE na katika hili Urasimu umepungua Sana kutofautisha na njia iliyotumika kwenye ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI ambapo ilifanya nafasi zitolewe kwa kujuana na hivyo wenye sifa kuenguliwa na wasio na sifa kupewa nafasi.
Ni ukweli usiosemwa lakini mchakato uliotumika kupata watu wa kwenye zoezi la ANUANI za makazi liligubikwa na utata usioelezeka na tulipoona application za ajira hizi za sensa zitafanyika ONLINE tukashukuru na kusema tatizo limetatuliwa lakini yanaenda yanaenda kujirudia yale yanayoumiza.
Kitendo Cha kuruhusu mchakato wa ajira za sensa kwa hatua ya mchujo kufanywa na watendaji wa kata/mtaa ni kuruhusu yaliyotokea kwenye ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI kujirudia, hivyo tunaomba Serikali itazame mchakato huu.
Kwa kuwa kila mtu aliyeomba nafasi hizo anajua ni mkazi wa eneo husika na fomu ya maombi inajieleza hakuna haja ya kutumia watendaji ili kuthibitisha ukazi wa muombaji. Yanayofanywa na watendaji yanaumiza maana bila koneksheni ni ngumu kupita kwao.
Mapendekezo:
1. Kama mnataka watendaji wawe sehemu ya mchujo basi msitumie watendaji wa eneo hilo kuchuja watu walioomba eneo hilohilo na badala yake kwa mfano watendaji wa wilaya ya masasi wanaweza kufanya mchujo wa waombaji wa tanga hii itapelekea Usawa ilhali hujuma haziwezi kukosekana.
2. Wakati wa usaili ,kwa kuwa tumeamua kutumia njia za kisasa wakati wa kufanya application basi twende na usasa huohuo kwa interview kufanyika ONLINE. Kufanya interview hiyo online itasaidia kupunguza upendeleo
Katika kufanya usaili online pia inaweza kuboreshwa watu wasailiwa wanaweza kukutana ofisi ya kata kwa ajili ya interview na unaweza kutengenezwa mfumo wa maswali ya interview ambao ili kuingia kwenye mfumo kushiriki interview lazima uwe na password na password hiyo inatolewa ofisini tu. Hii itafanya watu watumie simu zao kwa ajili ya interview lakini muda wa interview mfumo usiowaruhusu kutoka nje ya mfumo na wakifanya hivyo watakuwa wamejiondoa.