Ushauri kwa Serikali kuhusu muandamo wa mwezi

Nadhani hujanielewa sehemu, nimemaanisha leo sio siku ya mapumziko kisheria. Hivyo wanaosherehekea leo wanalazimika kwenda makazini. Ila kama serikali ingetangaza leo ni mapumziko basi na wao wangekuwa na muda mzuri zaidi

Halafu kwa ujuavyo serikali ni nani? Unavyoviona leo kama sheria/mifumo huko serikalini ni mawazo yaliyotolewa na watu kama mimi na wewe na yakafanyiwa kazi.

Kuhusu sayansi na teknolojia hapo ndipo unakosea sana, kwani aliyekupa ufahamu wa kuvumbua hizo sayansi na teknolojia ni nani? Kwahiyo wewe mpaka leo unapanda ngamia/punda kwenda kusalimia wazee wako kijijini huko?

Swali la mwisho, niletee hadithi zinazosema mtume Muhamad(SAW) alifunga/fungua ramadhan zote kwenye maisha yake kwa kuuona mwezi kwa macho yake bila kuambiwa.
 

Kabla Sijakuambia Hiyo Hadithi Naomba Unipe hiyo Hadithi au Aya Inayosema Mtume Muhammad (S.A.W) alifunga Au kufungua Kwa Kuambiwa na Watu waliouna mwezi Bila Yeye Kuthibitisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…