Ushauri kwa Serikali kupitia TANROAD, ni afadhali kutokujenga barabara za lami zenye kiwango cha chini mpaka pale budget kubwa itakapopatikana

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Ushauri kwa Serikali kupitia TANROAD, ni afadhali kutokujenga barabara za lami zenye kiwango cha chini mpaka pale budget kubwa itakapopatikana

Kujenga barabara za lami zenye kiwango cha chini cha ubora ni kuingiza hasara kwasababu italazimu kurudia kwa mara nyingine kwasababu ya kushindwa kudumu

Barabara zenye kiwango kidogo cha ubora zinaharibika ndani ya muda mfupi na ikiwa budget ilikuwa 1Billion kipindi zikijengwa basi kurudia kwa mara ya pili gharama zinakuwa juu kwasababu ya mabadiliko ya gharama za ujenzi ikiwemo malighafi

Lakini mbaya zaidi ni kuwa barabara zenye kiwango kidogo cha lami zinasababisha kutokukoma kwa kazi za ujenzi wa barabara kwasababu inalazimu kurudia mara kwa mara kwahiyo kazi ya ujenzi haikomi

Ikiwa kuna barabara zilizojengwa kwa kiwango kikubwa cha ubora matokeo yake ni kuwa hazitowahi kurudiwa tena kwahiyo inasaidia kulinda mfuko wa Serikali na kuelekeza budget kwenye maswala mengine badala ya ujenzi
 
Wazee wa 10% watakula wapi sasa??
 
Afrika Kila kitu ni kama cursed tu mvua ikinyesha mafuriko,isipo nyesha hakuna maji,Barabara nazo ndo hovyo kabisa holes Kila sehemu.

Njoo kwenye city planning sasa ndo kabisa.
Laana ipo ya uharibifu kwasababu kwa akili ya kawaida kiongozi hawezi kufanya utumbo
 
Barabara inatengenezwa hata mwaka haujaisha imesha chakaaa vibaya sijaju hua hakuna garantii kwenye barabara?Ukiacha hilo barabara inajengwa nyembamba baada ya miaka miwili wanaanza yena kuitanua unajiuliza hivi hawa mbona wanachezea hela hivi kwa nn wasinge jenga barabara yenye viwango tangu mwanzo
 
Ndo kosa wanalofanya na litawagharimu watajenga barabara zisizoisha hadi watakapozeeka
 
Kwani wanarudia kwa pesa zao za mfukoni??
Barabara kurudiwa kujengewa mara nyingi ndio faida zaidi kwao kwa sababu watakula hizo 10% mara nyingi zaidi.
Kweli Afrika laana ipo
 
Hizo sarakasi za ujenzi ndio chaka la upigaji la wahuni. Kujenga chini ya kiwango, kujenga kwa muda mrefu na kurudiarudia ndio upigaji unakuwa rahisi kwa watumishi wa ngazi za kati na chini.
 
Ndo kosa wanalofanya na litawagharimu watajenga barabara zisizoisha hadi watakapozeeka
Tatizo lipo kwa wananchi wa chini ndiyo watakaoteseka. Hao viongozi wao ni kunufaika na ubadhirifu wa pesa pia hata wakipita wanapita na gari za gharama na escort.
 
Ndo kosa wanalofanya na litawagharimu watajenga barabara zisizoisha hadi watakapozeeka
Kuna ile unakuta wamejenga vizuri lakini hata mwezi haujaisha unakuta kuna watu wanakata lami wanaweka
Ndo kosa wanalofanya na litawagharimu watajenga barabara zisizoisha hadi watakapozeeka
Kuna uhuni mwingi sana na sijui hawa watu kama wanauchungu na kodi zetu ukibahatisha barabara ambayo imejengwa ikadumu miaka miwli bila mashimo ni nadra sana
 
Laana ipo ya uharibifu kwasababu kwa akili ya kawaida kiongozi hawezi kufanya utumbo
Mafisadi hawagopi laana, Africa bila sheria kali za kunyonga na kufilisi mafisadi kama za China huwezi kupunguza ufisadi.
 
Tatizo sio budget, tatizo ni usimamizi mbovu hata wale wanaoenda kukagua mradi kabla haujakabidhiwa sijui huwa hawaoni na kingine me nadhani ni mikataba wanayosaini hao wakandarasi haiwabani unakuta barabara ina miaka miwili tu lakn imeshachakaa na bado mbunge anaenda kuomba fedha za ukarabati wa barabara ile ile
 
Afrika ni kichwa cha mwendawazimu
 

Attachments

  • 20260217_112940.jpg
    319.6 KB · Views: 29
  • 20260217_112932.jpg
    273.6 KB · Views: 32
Kwani wanarudia kwa pesa zao za mfukoni??
Barabara kurudiwa kujengewa mara nyingi ndio faida zaidi kwao kwa sababu watakula hizo 10% mara nyingi zaidi.
Wale watu sidhani kama bado wanakula 10%. Sasa hivi yawezakuwa washafikia kwenye 40% huko. Kama budget ilitengwa barabara iwe ya kiwango cha chini,basi itajengwa kwa kiwango cha hovyo kabisa.

Case study: Benjamin Mkapa studium
 
iyo miradi ya ujenzi ndo ya viongozi wetu kufanyia fraud kubwa kubwa wewe unataka isitekelezwe unafikiri watakuelewa?na tena wanafurahia ikitokea mara kwa mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…