Ushauri kwa Serikali kupitia TANROAD, ni afadhali kutokujenga barabara za lami zenye kiwango cha chini mpaka pale budget kubwa itakapopatikana

Ninafikiri kutokuwepo usimamizi mzuri na pia rushwa ni sababu kubwa. Niliwahi kusimamia barabara kwenye kitengo cha kuangalia viwango niliyoyaona basi tu. Bila kuwa mzalendo wa kweli na kuamua kuishi maisha ya kuridhika ni ngumu sana kukwepa vishawishi vya rushwa. Kutokuwepo uzalendo ni shida kubwa sana.
 
Barabara bora hujengwa kwa zege, ila la! Tatizo hazina ripea huku sisi tuna familia, tutaishije.
 
Hizo sarakasi za ujenzi ndio chaka la upigaji la wahuni. Kujenga chini ya kiwango, kujenga kwa muda mrefu na kurudiarudia ndio upigaji unakuwa rahisi kwa watumishi wa ngazi za kati na chini.
Kama ni hivyo basi hao viongozi ni wajinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…