Ushauri kwa Serikali: Riba na bima ya mkopo

Ushauri kwa Serikali: Riba na bima ya mkopo

Leele

Member
Joined
May 11, 2020
Posts
39
Reaction score
18
Serikali tangu awamu ya tano haipajandisha mshahara wala kulipa malimbikizo kwa watumishi hata hii ya sita japo inasema wamepandisha lakini ni ongezeko kidogo sana kiasi ambacho hakileti mabadiliko yoyote kwa maisha ya mtumishi japo gharama zinabadilika kila uchao. Pamoja na hayo watumishi wameendelea kuwa waaminifu na kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu.

Tumeona baadhi ya mabenki yakishusha kiasi cha riba lakin kitu cha ajabu sana unakwenda kuchukua mkopo pamoja na riba kuwa chini ila shida inakuja unatakiwa ulipe bima ya mkopo kwa mkupuo mmoja jambo hili linaumiza sana japo kabla ilikuwa inalipwa kidogo *2 mpka mkopo unaisha?

Serikali tafadhali ondoeni utaratibu was kulipa bima ya mkopo kwa Mara moja utaratibu huu so rafiki kabisa kwa mtumishi no kandamizi kabisa. Ujumbe uwafikie wahusika.
 
hivi bima ya mkopo ina maana gani haswa na faida yake ni nini? Kwamba mkopo ukiisha bila sababu za kukopea kukamilika unapewa nyingine au fedha ya mkopo ikiibiwa unalipwa nyingine?!!!
 
hivi bima ya mkopo ina maana gani haswa na faida yake ni nini? Kwamba mkopo ukiisha bila sababu za kukopea kukamilika unapewa nyingine au fedha ya mkopo ikiibiwa unalipwa nyingine?!!!
Ukifa/ukipata ulemavu wa kudumu Deni Lako atalipa Nani?

Kwani insurance ya Gari/chombo Cha moto hua ikiisha na Gari halijata madhara yoyote Yale ya kulipwa na bima,then hio pesa uliyolipa bima hua unai-carry forward au unalipa upya insurance?
 
Huo ni upigaji kama upigaji mwingine
Ila umejificha kwa mgongo wa bima ya mkopo.Mabenki yanatuibia kisomi hapo. Natamani huu uwe mjadala mkubwa hapa jamvini na ikiwezekana tuandamane mpaka Ikulu.
 
Back
Top Bottom