Ushauri kwa Simba: Kipigo Cha Leo kitutoe usingizini.

Ushauri kwa Simba: Kipigo Cha Leo kitutoe usingizini.

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Naomba kuwapa pole mashabiki wa Simba kwa kipigo Cha Leo. Sio lelemama.

Kutokana na kipigo hicho Simba inatakiwa ikitumie kipigo hicho Kama changamoto ya mabadiliko. Ila Simba Kama Klabu ikichukulia kipigo hiki Kama kawaida, basi yatakuja makubwa zaidi.

Naomba nishauri yafuatayao:

1. Kwanza, Simba iwekeze kwenye kutengeneza kikosi Bora, iachane na propaganda. Kwa maana isajili wachezaji wanaojituma. Tuachane na kukalili majina kwamba lazima Mohamed husein au Kapombe lazima acheze. Huo ni ujinga. Tujenge timu inayotisha sio majina ya wachezaji.

2. Kusajili kocha mwenye mbinu na ubora. Hapa nisema tusisajili kocha kwa kwa kuangalia rangi yake ya ngozi

3. Viongozi kutoridhika hapa ilipofika Simba na kuiangalia Simba Kama Timu Kubwa. Ni Kama Viongozi wameridhika haraka kwa mafanikio waliyopata Simba huko nyuma na hawataki kubadilika au kuja na plan ya miaka mitano ijayo.

4.Viongozi wa Simba wapunguze propaganda zisizokuwa na maana. Nakumbuka uchaguzi wa mwisho, Viongozi wa Simba walimleta Manzoki , sikuelewa walikuwa na maana gani, ila baada ya uchaguzi Manzoki hakuongelewa Tena.

5. Viongozi waache kutembelea historia. Nilimsikia Mwenyekiti wa bodi, Salim Try again akidai watu wanalalamika kwa sababu Simba ilikuwa inashinda huko nyuma. Nikawaza kwa hivyo Simba ikishinda huko nyuma kwa Sasa haitakiwi kushinda?.

6. Mwisho, Wanachama wa Simba tuchague Viongozi wenye vision, sio wanaokuja kutafuta umaarufu Simba au kutumia Simba Kama ngazi ya kupandia kwenda kwenye ubunge.

Tusipoanagalia haya, Simba itashuka na itakuwa kazi kuinyanyua.
 
Tulia mkuu, kunywa maji nafsi ipumue.

Ukizoea kupata jua kuna kukosa pia, hivyo shusha pumzi.
Umeongea kwa hisia kali sana ila tegemea propaganda kuendelea badala ya kuboresha.


"Simba guvu moya"
 
Tatizoa simba linaanzia kwenye uwekezaji,ni ujanja ujanja wa gabachori hamna kitu pale
 
Propaganda nyingi msimbazi.

Wazee wa Mo wamesaidia nini? Ukiona propaganda nyingi ujue kuna upigaji na mambo hayako sawa.
 
Back
Top Bottom