Ushauri kwa TANROADS

Ushauri kwa TANROADS

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Nimepita daraja la Wami Dakawa, nikapita daraja la Ferry Dumila, nikapita madaraja ya Kitete, Msowero, Mvumi na Rudewa barabara ya Dumila Kilosa nikajifunza kuwa madaraja ya njia hiyo yaliinuliwa juu sana kiasi kwamba siyo rahisi kuathiriwa na mafuriko ikiwa mvua kubwa zitanyesha Kiteto, Gairo na kwingineko.

Ushauri wangu ni kuwa ijengwe barabara ya dharura yenye madaraja yaliyoinuka kama yale ya Kilosa kuanzia Rudewa hadi Mangae au Melela Mlandizi ili ikitokea madaraja ya Ferry na Wami (Morogoro to Dodoma Highway) yamekatika au kufunikwa na mafuriko, iwe rahisi kuhama njia na kupita Morogoro -Iringa Highway.

Nb.
Tukosoane kiistaarabu siyo matusi
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom