Agresive
JF-Expert Member
- Feb 18, 2018
- 890
- 1,236
Ni weekend nyingine wakuu natumaini mu-wazima wa afya.
Kuanzia 2015 mpaka sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wadahiliwa kukosa vyuo au kozi ya ndoto yake ingawa kuwa ufaulu wake unajitosheleza kujiunga na kozi husika sababu kuu za kukosa zinaweza kuwa:
1. Ushindani mkubwa kwa kozi husika
2. Kuongezeka kwa idadi ya wahitimu dplm na form six
3. Kasi ndogo ya vyuo vikuu vipya kuongezeka
4. Kufungiwa au kuzuiliwa udahili vyuo vikuu baadhi.
5. Uwezo mdogo wa vyuo kudahili watu kutokana na nafasi kuwa chache kwa kozi husika.
6. Mifumo mibovu ya udahili au TCU kutokujipanga vyema wakati wa udahili. Mfano isue ya CODES ZA KUCONFIRM.
Na sababu kama hizo.
USHAURI:
Vyuo vikuu vingi ukifatilia vinatoa Elimu ngazi ya CHETI, DPLM DEGREE NA KUENDELEA. Inawezekana siku za nyuma walifanya hivo ili kuepuka kutokujaza chuo kwa kutegemea watu wa kusoma degree tu.
Umefika muda muafaka TCU NA WIZARA YA ELIMU wafanye uchunguzi na maamuzi kuwa VYUO VYENYE HADHI YA KUTOA DEGREE VITOE DEGREE TU NA KUONDOA KOZI ZA CHETI NA DPLM ILI VYUO VIWE NA UWEZO MKUBWA WA KUDAHILI WAHITIMU WA FORM 6 NA DPLM.
Ngazi ya cheti na dplm zibakie kutolewa kwa vyuo vya hadhi ya kutoa ngazi hizo tu..
Zamani kukosa chuo kilikuwa kinaonekana ni kitu hakiwezekani lakini kuanzia mwaka jana isue ya kukosa chuo imeanza kuwa tatizo na mwaka hadi mwaka tatizo linaongezeka.
Zaman mtu aliyesoma PCB hata awe na dvsn 3 alikuwa na uhakika wa kusoma MD lakini mwaka huu kuna watu wamesoma PCB ana dvsn 1 au 2 wamekosa nafas za MD kwa kigezo cha ushindani, unakosa nafas wewe wa MD hlf chuo kinachotoa kozi yako kimejaza watu wa cheti na dplm.
Sijaandika kwa ubaya kuwa watu wa cheti au Dplm hawapaswi kusoma isipokuwa chuo cha degree kitoe degree tu na chuo cha Dplm au cheti kidahili watu wa ngazi hiyo tu.
Pia serikali ijipange kujenga chuo kingine kikubwa kama UDOM siku za usoni ili kukabiliana na wimbi la wanachuo kukosa vyuo, piga picha miaka 15 mbele hali itakuwaje?
MWISHO. serikali pia ipitie. ADA ya vyuo vikuu vya serkali zinatofautiana sana mfano UDOM kozi ya elimu laki 7 wakati MZUMBE kozi hiyo hiyo ya ELIMU milion 1 na laki 3. hlf vyote ni vya serikal huo utofauti ni mkubwa sana.
Pia wajitahidi kujenga HOSTEL kwa vyuo ambavyo hostel hazitoshelezi watu wanakimbilia UDOM kwa sababu ya unafuu wa maisha HOSTEL ZIPO ADA NAFUU.
Nawasilisha na samahan kwa uzi mrefu.