Ushauri kwa TFF: Mnapopanga ratiba za saa nane mchana, hakikisheni Kila timu inaguswa na hiyo ratiba

Ushauri kwa TFF: Mnapopanga ratiba za saa nane mchana, hakikisheni Kila timu inaguswa na hiyo ratiba

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Ushauri huu ufike moja kwa moja katika shirikisho la mpira Tanzania (TFF), nilikua naangalia ratiba za wenzetu waliotuzidi kimaendeleo ya mpira wa miguu, nikili tu kiukweli ratiba zao hazina upendeleo haswa kwenye suala muda.

Iwe man u, iwe na Manchester city ratiba ya muda Kama ni mchana basi ratiba itakugusa haijalishi wewe ni mkubwa kiasi gani na hiyo ndiyo mantiki ya shirikisho la mpira kutoingiliwa katika upangaji wake wa ratiba labda itokee dharura.

Sikumbuki ni lini timu zetu kongwe(Simba na Yanga) zilicheza saa nane mchana sikumbuki kabisa na Kama walicheza basi ni muda mrefu sana.

Ukizitoa Simba na Yanga kutocheza saa nane mchana jua Kali likiwaka timu zilizobaki zote huwa zinaguswa na hiyo ratiba ya saa nane mchana, sijui ni kipi huwa kinatazamwa.??

Nikisema ni upendeleo nitakua nimekosea?? Je hao wanaochezeshwa mchana wakati wengine ratiba hiyo haiwagusi, je wanajisikiaje???

Najua Simba na yanga siku wakichezeshwa saa nane jua Kali Kuna wachambuzi, wanasayansi mpaka wataalamu wa jua wataibuka kuzitetea timu zao pendwa Ila kwa Sasa wapo kimya tu.

My take, TFF guseni ratiba ya mchana kwenye timu zote siyo ihefu, ruvu nk

Imeandikwa na NALIA NGWENA
 
Mechi ya Simba na Yanga ina mengi nyuma, Moja ni Biashara. Hizi mechi huwa zinapangwa kuhakikisha Mapato yanakusanywa kwa wingi sana,mfano kutanua wigo wa wahudhuriaji.
 
Mechi ya Simba na Yanga ina mengi nyuma, Moja ni Biashara. Hizi mechi huwa zinapangwa kuhakikisha Mapato yanakusanywa kwa wingi sana,mfano kutanua wigo wa wahudhuriaji.
Nini maoni yako aisee.
 
Lakini siyo SAWA. mtoa mada katoa mfano mzuri wa sana wa Ligi ya Uingereza!!
Sasa mkuu ligi ya uingeleza sawasawa na huku kwetu , timu zinazoingiza mapato pale TFF ni mbili tuu simba na yanga na ndomaana zinalindwa sana , kule uingeleza kila timu inajiweza FA hawategemei timu moja
 
Bado haijawa sababu ya kutokuzipanga hizo timu mchana. Wenyewe mechi za Dar zaidi ya "Deby" hakuna mechi nyingine wanazoingiza hela nyingi. Kwani simba na Yanga zinapocheza na KMC huwa zinakuwa na mashabiki wengi uwanjani??

Wapangwe kucheza mchana!
 
Mkuu hata hivyo ishu ni suala la match coverage kwenye TV ndo inasababisha yote haya, ndo maana siku hizi imepungua baada ya viwanja kadhaa kuwekwa taa na kutumika usiku.

Kingine ukweli utabaki pale pale timu za dar zile 2 zinamashabiki wengi sana. Wataalam wanakwambia ukiweka muda mzuri kama jioni au usiku basi watu wengi wataona mchezo na matangazo yatalipa so ni ishu ya biashara, sikumbuki lini nimeangalia game wanacheza kmc na mbeya city.

Ma"gap" hayaepukiki.
 
Mkuu hapo kuna sponsors ambaye ananufaika na wanaoziangalia hizo game hata ulaya game za saa sita ambazo ni weekend na mara nyingi ni derby waliziweka hivyo ili watu wawe hawajapiga kinywaji na kuleta fujo na game mara nyingi ya baadae sana inakuwa na viwership ya average ili wengi waione baada ya mechi nyingi, nyingine....

Vilevile kila siku huwa kunakuwa na Match of the Day ambazo hizi inapewa karibia kila atleast mara moja (kila mwenye package ya kawaida anaweza kuona) ingawa kama una pesa zako mechi yako unaweza ukaitafuta kwenye channels nyingine..., ila kama unacommand viewership kubwa lazima muda wako utakuwa favorable na wengi wakuone

In short katika kupanga ratiba sio TFF pekee hata sponsor anayetaka kuonyesha hizo game ana say na say yake hio ipo pale angalau return on investment yake isiwe negative sana....; huenda wewe kucheza kwako saa nane wengi wakakuangalia kuliko ungecheza wakati wengine wanacheza basi huenda hata mashabiki wako wasikuangalia waangalie big teams
 
Ushauri huu ufike moja kwa moja katika shirikisho la mpira Tanzania (TFF), nilikua naangalia ratiba za wenzetu waliotuzidi kimaendeleo ya mpira wa miguu, nikili tu kiukweli ratiba zao hazina upendeleo haswa kwenye suala muda.

Iwe man u, iwe na Manchester city ratiba ya muda Kama ni mchana basi ratiba itakugusa haijalishi wewe ni mkubwa kiasi gani na hiyo ndiyo mantiki ya shirikisho la mpira kutoingiliwa katika upangaji wake wa ratiba labda itokee dharura.

Sikumbuki ni lini timu zetu kongwe(Simba na Yanga) zilicheza saa nane mchana sikumbuki kabisa na Kama walicheza basi ni muda mrefu sana.

Ukizitoa Simba na Yanga kutocheza saa nane mchana jua Kali likiwaka timu zilizobaki zote huwa zinaguswa na hiyo ratiba ya saa nane mchana, sijui ni kipi huwa kinatazamwa.??

Nikisema ni upendeleo nitakua nimekosea?? Je hao wanaochezeshwa mchana wakati wengine ratiba hiyo haiwagusi, je wanajisikiaje???

Najua Simba na yanga siku wakichezeshwa saa nane jua Kali Kuna wachambuzi, wanasayansi mpaka wataalamu wa jua wataibuka kuzitetea timu zao pendwa Ila kwa Sasa wapo kimya tu.

My take, TFF guseni ratiba ya mchana kwenye timu zote siyo ihefu, ruvu nk

Imeandikwa na NALIA NGWENA
Ratiba haipangwi na TFF pekee
Azam TV, TFF, wenye viwanja vyao na timu zinazoshiriki zinahusika. Ndiyo maana husikii wakilalamika
 
Ratiba haipangwi na TFF pekee
Azam TV, TFF, wenye viwanja vyao na timu zinazoshiriki zinahusika. Ndiyo maana husikii wakilalamika
Kwa unataka kusema hao Azam wanapenda kucheza saa nane mchana, ruvu na polisi

Sikubaliani na wewe unachokisema kwamba timu zinashiriki kupanga muda wa kucheza Ina maana timu kumi na nne zote zinapenda kucheza saa nane mchana???
 
Back
Top Bottom