Pre GE2025 Ushauri kwa vyama vyote kuhusu uteuzi wa viti maalum kwa wanawake, muhula mmoja unatosha kuwapa uzoefu wa kugombea

Pre GE2025 Ushauri kwa vyama vyote kuhusu uteuzi wa viti maalum kwa wanawake, muhula mmoja unatosha kuwapa uzoefu wa kugombea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Ni jambo la busara kuwawezesha akina Mama katika uteuzi wa viti maalum Bungeni. Wanapokuwa Bungeni wanapata uzoefu jinsi ya kuongoza na kuishi na jamii kwa ujumla.

Pamoja na mazuri yote wanayofanya akina mama wanaoteuliwa kwa njia ya Viti maalum NINAPENDEKEZA kuwa uteuzi wa Viti Maalum kwa akina mama udumu kwa muhula moja tu wa Bunge yaani miaka mitano na kuwaachia wengine pia waingie Bungeni kupata uzoefu.

Napendekeza kuwa wale waliomaliza miaka mitano Bungeni na tayari wamepata uzoefu sasa warudi kwenye Majimbo na kuchukua fomu ili wapambane kama ilivyo kwa wanaume.
 
Ni jambo la busara kuwawezesha akina Mama katika uteuzi wa viti maalum Bungeni. Wanapokuwa Bungeni wanapata uzoefu jinsi ya kuongoza na kuishi na jamii kwa ujumla.

Pamoja na mazuri yote wanayofanya akina mama wanaoteuliwa kwa njia ya Viti maalum NINAPENDEKEZA kuwa uteuzi wa Viti Maalum kwa akina mama udumu kwa muhula moja tu wa Bunge yaani miaka mitano na kuwaachia wengine pia waingie Bungeni kupata uzoefu. Napendekeza kuwa wale waliomaliza miaka mitano Bungeni na tayari wamepata uzoefu sasa warudi kwenye Majimbo na kuchukua fomu ili wapambane kama ilivyo kwa wanaume.
Viti Maalumu vya Kuteuliwa kutoka Majimboni havina UMUHIMU tena kwa sasa, imepitwa na wakati.

Tubadilishe Katiba ya nchi ili Wabunge watokane na mikoa, kila Mkoa utoe Wabunge wa kuchaguliwa wapatao wawili au wanne, yaani Wabunge Wanaume Wawili na Wabunge Wanawake pia wawe wawili. Kusiwepo na Wabunge wa Viti Maalumu wa kuteuliwa Kutokea Majimboni au wa kuteuliwa kutoka kwenye Uwakilishi wa Majimbo au Mikoa.

Rais wa nchi apewe nafasi zake Kumi tu (10) za kuteua Wabunge wa Kuteuliwa, pasiwepo na idadi nyingine zaidi ya Wabunge wa kuteuliwa zaidi ya hao Kumi wa kuteuliwa na Rais wa nchi.
 
Back
Top Bottom