Ushauri kwa wachumba wanaotaka kuja kuwa wanandoa

Ushauri kwa wachumba wanaotaka kuja kuwa wanandoa

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Leo niwashauri wale ambao hamjaoa au kuolewa ila mpo kwenye mahusiano sijui uchumba au nini:

Onyesheni zile tabia zenu halisi, yaani usiigize chochote, kama wewe unakula sana, kula, kama wewe huwa unaoga kwa wiki mara moja tu basi fanya hivyo, kama huwa husalimii watu basi endelea. Yaani kila tabia yako muonyeshee huyo 'baby' wako.

Hata mkija kuoana mtaishi maisha yale yale tu, tena hutapata shida!

Kuna watu waliigiza kwenye uchumba, sasa kwenye ndoa ndiyo wapo nyuma ya pazia!

Narudia tena, kama unavuta bangi zako, basi vuta huyo mpenzi wako akiwepo au ajue kabisa unavuta bangi. Kama wewe huwa unatukana au kuchamba wamama watu wazima basi usijizuie eti kisa mpenzi wako yupo!

Narudia tena kila mtu na mtuwe! Usiigize wala kuigiza maana baadaye utakuja kupata shida sana kuishi katika uhalisia wako! Wacha ajue tabia yako mapema ili aamue kusuka au kunyoa.

Mkienda kwenye ndoa ni kwamba tayari mmekubaliana na jinsi mlivyo!
 
Huyo ni mimi kabisa, katika ushauri huu ni mimi huyo sinaga muda wa ku-fake maisha, consequences zake ni mbaya sana kuna ndugu yangu anajuta sasa baada ya ku-pretend kwa muda sasa anasaga meno
 
Kuna mwamba alitrend kwenye mtandao wa Instagram...akimwambia mtarajiwa wake "sitaki show off " ...[emoji2][emoji2],
 
Ukwel mchungu ...!! Kuna mtu ana gubu huyo mwanzoni hakua hivyio Sasa mke anakoma kitu kidogo ni kurap hadi albam inakAmilika.
 
Back
Top Bottom