Ushauri kwa wadada wote wanaotumia rangi ya mdomo, zina madhara

Paka mafuta.. Chora na wanja.. Ni basi tu wanaume hawana nongwa.. Ila mtu unamkuta na domo jekunduu km kidonda.. Siwasemi ubaya sema ukiwa tu msafi inatosha.. Hayo ma lipstick hata sio kiviiile.
Hivyo wanja hauna tatizo kiafya Mkuu?

Hahahaaa. Ila ni ngumu aisee kwa mfano unakwenda kwenye sherehe kwa usiku mmoja ndani ya Wiki sidhani kama domo kuwa jekundu kwa muda ni mbaya sababu tukishatoka shereheni tunaoga na kutoa mirangi yote.

Pia niseme Mkuu lipstick haifanyi mwanamke akawa mchafu bwana.
 
Mie pia mtu wa Pwani Mkuu ndio sababu nikasema sikumaanisha hayo.

Kwaheri. [emoji124] [emoji124] [emoji124]
Sijakugomba nimekwambia tu, mimi ni mtu wa pwani tena Muislamu.
Na wewe nimehisi kama ni Muislamu
 
Hatupingi ila tumewaona Mama zetu wanawaka waka na wala hakuna Lipstick saana wanja ambao ni ranging nyeusi na mafuta sio?

Hakuna kitu kizuri kama kuonekana mrembo ukiwa karibia na uasilia wako hii ppda mpaka unakuwa kama ubao wa shule na nywele za katani kama umebeba mzigo.

Hizi rangi zikiwa zinaelekea na uasilia mnapendeza zaidi na huenda zinakuwaga ghali pia maana unawaona wanaojielewa sana tu ndio wanazitumia.

Sasa kweli ukawe na mdomo wa zambarau, mwekundu, wa blue, wa rangi ya kitu mara kijani njano binaadamu wa namna gani huyo mama?

Hahaha, muweke mafuta tu mbona mnapendeza sana hizi rangi nyingine zinaonekana way unnatural wao huko ulaya wengine wana midomo myekundu sasa tusiige Mungu fundi huwezi kumkuta mtu anakucha nyeusi na macho mekundu na akawa na afya njema kila kitu kina hue and shades na mungu amezingatia.

Pigeni chini hayo madubuwasha weka mafuta ukiongeza weka nywele za uzi swaaaafi kabisa hayo madude ya midoli waachieni hao wazungu.

😉
 
Lipstick ni kiboko kwa kuharibu ndoa za watu hasa wanaume wachepukaju,akienda kwa kimwali kingine kinamkiss begani haha akirudi kwa mkewe anaulizwa hii lipstick kwenye shati umetoa wapi,na hapo ndo vita ya tatu ya dunia inapoanza
Hahaa ukiwa sungura mambo kama hayo unapangua vizuri tu bila tabu.
 
Sawa Mkuu ahsante kwa ushauri. Pia nadhani kwa ulichoandika watakuelewa wengi japokuwa nje ya lipstick hivyo vingine naviona kwa marafiki tu sababu sina ushabiki navyo.

Ila nimecheka lol "eti tupeni chini hayo madubwasha" hahahaaa.
 
Insh'Allah Mwenyezi Mungu akufanyieni wepesi mrejeshe nuru ya uafrika halisi
naona kalipstik umekafanyia mgomo. 🙂
 
Insh'Allah Mwenyezi Mungu akufanyieni wepesi.. mrejeshe nuru ya uafrika halisi.
Naona kalipstik umekafanyia Mgomo. 🙂
Amiin. Insha Allah. [emoji120] [emoji120] [emoji120]

Hahahaaaa. Nitapunguza kidogo ila sio kuacha kabisa Mkuu.
 
Aiseeh hiyo kitu kupaka mdomoni ilinishinda kabisa, nilishawahi kujaribu kwa kufata mkumbo wa marafiki lakini niliishia kujifuta tuu. Kwanza nikikutana na mtu akanitazama uwiii najiskia vibaya naona kama nimekuwa kituko fulani.

Mie mafuta na wanja kwangu burudani kabisa ila wakipaka wenzangu naona wanapendeza kwelikweli, labda ni kwasababu sio kila kitu ni kwa ajili ya kila mtu.
 
Mmh! Mie bado kushawishika kuacha kwa kweli sababu mizunguko yangu yote lazima lipstick ihusike.

Mie nadhani mtushauri tusipake mara kwa mara na sio kuacha kabisa sababu mkisema tuache tofauti ya mdomo wa mwanaume na mwanamke itakuwa wapi.
Mdomo wa mwanaume haufananagi na wa mwanamke, madam!!
 
Wengi wanaopaka ni waliosoma art
 
Paka mafuta.. Chora na wanja.. Ni basi tu wanaume hawana nongwa.. Ila mtu unamkuta na domo jekunduu km kidonda.. Siwasemi ubaya sema ukiwa tu msafi inatosha.. Hayo ma lipstick hata sio kiviiile.
Yani maliplistick yanabore !
 
Mmh! Mie bado kushawishika kuacha kwa kweli sababu mizunguko yangu yote lazima lipstick ihusike.

Mie nadhani mtushauri tusipake mara kwa mara na sio kuacha kabisa sababu mkisema tuache tofauti ya mdomo wa mwanaume na mwanamke itakuwa wapi.
Ha ha ha ha ha nimecheka hapo kwenye tofauti ya mdomo wa KE na ME.
Umetisha...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…