Ushauri kwa wanachama wa Yanga kuhusu Manji kukodisha timu kwa miaka 10

Ushauri kwa wanachama wa Yanga kuhusu Manji kukodisha timu kwa miaka 10

koryo 2

Member
Joined
Jul 29, 2016
Posts
24
Reaction score
12
Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni mpenzi wa Yanga. Mimi nakubaliana na Manji kukodisha Timu kwa miaka 10 ila Wanachama wazingatie yafuatayo:-

(1) Kuna uwezekano kwenye biashara kukawa na HASARA. Kiwepo kipngele kwenye mkataba kuwa Manji akipata hasara sharti awalipe Klabu Tshs.200,000,000 kila mwezi. Hii isiwe na mjadala.

(2) Kuilipa Klabu Tshs.250,000,000 kwa mwezi mimi kwangu naona ni kiduchu. Kiwepo kwenye mkataba faida inayopatikana iwe ni kwa njia ya wazi ambapo mahesabu yatapigwa na kufikia hiyo faida. Mahesabu yasifanyike kwa kificho. Nashauri Manji ailipe Klabu Tshs. 500,000,000 kwa mwezi na siyo Tshs.250,000,000 kwa mwezi.

(3) Wakati wa kuandika Mkataba Klabu ikodi Mwanasheria Nguli ili kusimamia mkataba huo na kuishauri Klabu. Nampendekeza Klabu impendekeze Wanasheria kama Ndugu Kibatala au T. Lissu.

(4) Ukaguzi wa mahesabu yasimamiwe Mashirika kama PriceWaterhouse au ErnstYoung ili kupata ukweli.

(5) Nawashauri Wananchama kuwa siyo wazo linaloletwa mbele yenu ni kuitikia NDIYOO............. hapana. Pokeeni wazo mlitafakari kwanza na baadaye kulitolea uamuzi. Zama za Ndiyooo............. zimepitwa na wakati.
 
TZ tumekalia porojo sasa wenzetu walishaanza kukimbia sisi tunajifunza kusimama katika umri uleule. Hii inapelekea haya yote kutokea hata anayekunyang'anya chako unabakia kuitikia tu na usijue la kumfanya! Ujinga, ujinga, ujinga ...tungeliupinga na elimu, elimu, elimu! Sasa hiyo elimu hatuna acha ujinga utumalize!
Naandika kama mtu aliyekata tamaa kwa maana hata wanachama wachache waliopinga hiyo juzi walizidiwa nguvu na kufukuzwa uanachama papo hapo, kielelezo kuwa tz ujinga una nguvu kuliko uelewa!
 
Acha kuwa na ndoto za mchana ndugu yangu, hatuhitaji mtu mwenye pesa kuja kujinufaisha kupitia wanachama kutangaza biashara zake, tunahitaji mtu mwenye vision za kibahresa awekeze kwenye soka za vijana, timu iwe na viwanja vyake/ academy, aweke wataalamu wa kutosha ikiwezekana kutoka nje ya nchi, timu ziwe na wadhamini wengi,. Hapo ndo tuanze kuongea kuhusu faida na hasara. Ila kuongelea faida sa hivi wakati mtu unampa timu yenye jengo linafurika maji wakati wa masika afu unasema akuletee faida Milioni 500,000,000.00 kwa mwezi, huo ni ukilaza wa mwendokasi.

Takupa mfano, wakati CRDB inaanzishwa watu walinununua hisa kwa wakati ule ilikua pesa ndogo sana efu 10 kwa hisa moja, baada ya watu kutoa pesa zao bank ikawa kama imeingia mitini, ikajijenga, kujizalisha watu wakajua wametapeliwa pesa zao, after 10 years wakaanza kugawa faida kwa wenye hisa na thamani ya hisa ikapanda mara dufu huku kukiwa na unafuu wa hisa kwa wale waanzilishi, kwa mtu aliyenunua hiza za elfu 50 mwaka 1996 leo hii hiza zake zina thamani zaidi ya milioni 25.

Tunahitaji mtu atakayejenga misingi imara ya club kiuchumi, ili tunapokuja kupata mafanikio yawe mafanikio ya kweli.
 
Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni mpenzi wa Yanga. Mimi nakubaliana na Manji kukodisha Timu kwa miaka 10 ila Wanachama wazingatie yafuatayo:-

(1) Kuna uwezekano kwenye biashara kukawa na HASARA. Kiwepo kipngele kwenye mkataba kuwa Manji akipata hasara sharti awalipe Klabu Tshs.200,000,000 kila mwezi. Hii isiwe na mjadala.

(2) Kuilipa Klabu Tshs.250,000,000 kwa mwezi mimi kwangu naona ni kiduchu. Kiwepo kwenye mkataba faida inayopatikana iwe ni kwa njia ya wazi ambapo mahesabu yatapigwa na kufikia hiyo faida. Mahesabu yasifanyike kwa kificho. Nashauri Manji ailipe Klabu Tshs. 500,000,000 kwa mwezi na siyo Tshs.250,000,000 kwa mwezi.

(3) Wakati wa kuandika Mkataba Klabu ikodi Mwanasheria Nguli ili kusimamia mkataba huo na kuishauri Klabu. Nampendekeza Klabu impendekeze Wanasheria kama Ndugu Kibatala au T. Lissu.

(4) Ukaguzi wa mahesabu yasimamiwe Mashirika kama PriceWaterhouse au ErnstYoung ili kupata ukweli.

(5) Nawashauri Wananchama kuwa siyo wazo linaloletwa mbele yenu ni kuitikia NDIYOO............. hapana. Pokeeni wazo mlitafakari kwanza na baadaye kulitolea uamuzi. Zama za Ndiyooo............. zimepitwa na wakati.
Kabla ya manji mbona hamkufanya yote hayo? Mmewahi pata faida kiasi gani kwa mfano!? Majungu
 
Watanzania kwa figisu Tambwe Leya alifundisha miaka2 bila mshahara leo ametokea mtu mwenye mapene mnachonga!
 
Yanga ni yetu watuachie sisi na Manji saafi siyo kama wale wanaogawana pesa za mauzo ya wachezaji halafu kutwa wanaomba michango kwa ajili ya usajiri.miaka 80 na ushee tumefaidika nn cha mno hadi tuone Manji anatulipa kidogo?
 
Umbea....umbea.....umbea.....umezidi,macho hayaoni mbali,midomo imepinda kwa kusema ya wenzenu,misikio waluwalu kwa kusikiliza ya wenzenu
 
Back
Top Bottom