David M Mrope
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 115
- 74
Ni jambo gumu sana kuwaelimisha hawa vijana lakini ni lazima tuseme kitu juu yao. Maisha ambayo wanayaishi chuo asilimia kubwa ni maisha yasiyo na mwelekeo bora,japo yanaweza kuwa sahihi kwao.
Yapo mambo mengi ambayo kijana wa chuo kikuu anapaswa kuyaelewa kuhusu maisha ili yamsaidie kuwa katika nafasi mzuri hapo baadae ambayo hatojutia. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo wanatakiwa wayazingatie sana.
(i) AFYA.
Hiki ni kitu muhimu sana katika dunia ya sasa, ambayo imekuwa ikikumbwa na majanga mengi baadhi ya hayo yakiwemo na milipuko ya magonjwa. Hawa vijana wetu wengi wao wamejisahau kabisa,kwao elimu kuhusu afya zao wanapuuza tu. Wengi hutumia mitandao ya kijamii kuomba ushauri wa magonjwa na kujikuta wakiandikiwa dawa ambazo huongeza madhara zaidi.
Vijana wengi kutokana na msukumo rika wamejikuta wakishawishiana kufanya mambo ambayo kiafya ni hatari zaidi. Wapo wanaotoa mimba,wapo wanaotumia vilevi vikali,wapo wanaotumia dawa za kuzuia mimba mara baada ya tendo (P2) n.k na hayo yote huona ni kawaida sana.
Vijana wa vyuo vikuu wanapaswa kujua afya ni kitu muhimu sana,afya ni zawadi bora sana,hivyo ni vizuri tukitunza afya zetu.
(ii) MIPANGO NA MALENGO.
Malengo ni kitu ambacho kila mmoja huwanacho kichwani, lakini lengo linapokosa mipango hugeuka kuwa ndoto tuu,tena zile za mchana. Mipango ndio njia ya kufikia malengo. Vijana wangu wa vyuo vikuu hili swala wanaliona si la msingi.
Mipango na malengo itakusaidia kuandaa mapema njia mbadala ya kupita endapo elimu uliyoisomea haitokusaidia kitu. Kwa sasa tunakabiriwa na changamoto ya ajira,ni vizuri kila mwanachuo kabla hajamaliza tayari kichwani mwake awe anampango B.
Hii itawasaidia sana kuto poteza muda mwingi baada ya kumaliza chuo katika kuwaza nini wafanye.
(iii) UHUSIANO BORA NA JAMII.
Hiki kipengere kinashangaza sana,vijana wengi wa vyuo vikuu wanasahau shughuli za kijamii na kuona haziwahusu. Wengi wao hulewa sana na sifa na kuona hawashahili kuwa pamoja na baadhi ya makundi ya watu hata katika shughuli za kijamii.
Vijana wanapaswa wajue kuwa,kuhudhuria mazishi,sherehe zozote,arobaini,kuona wagonjwa n.k ni jambo muhimu sana katika jamii. Wengi wao wakifika nyumbani basi wanajikita zaidi kutafuta pesa na kufikiri wale wanofanya shughuli hizo hawajui jinsi ya kuzitafuta hizo pesa.
Ni vizuri elimu zaidi ikatolewa kwa hawa ndugu zetu kuhusu hizi shughuli za kijamii kwa sababu wasomi wanaongezeka na hizi tabia hii inashamiri zaidi mitaani kwetu.
(iv) TAMADUNI.
Hili pia ni jambo ambalo kwa kiasi kikibwa linaenda kupotea. Lengo kuu la tamaduni za kiafrika zilikuwa ni kuunganisha jamii kuwa kitu kimoja na kuishi kwa amani. Zamani waliishi kwa upendo,amani na waliishi pamoja. Walisaidiana kupambana na njaa,mafuriko, magonjwa na hadha zote.
Kadri siku zinaenda utandawazi ukaingia hasa vyuoni,na wanachuo wanaongezeka. Basi elimu wanazozipata zinaanza kuwalainisha taratibu na kuona kwamba ule umoja waliokuwa nao wazee wao ni umaskini na utajiri ni kila mmoja kuishi kipeke yake.
Hili jambo ni muhimu tukiwafundisha vijana kuwa tamaduni zetu hudumisha umoja. Leo hii kijana akimaliza chuo hata watoto wa shangazi zake hawafahamu.
(v) IMANI.
Wengi wa vijana hawa walikuwa ni wale waliosifiwa kwa tabia njema wakati wapo shule za msingi. Wengine waliendelea kusifiwa hata na viongozi wao wa dini. Waliendelea kusifiwa ni vijana mahili kwa kipindi chote.
Walipofika chioni akili zikaanza kuwaambia kuwa habari ya Mungu ni jambo la hiyari. Wamesahau kuwa wazazi wao waliwalea ili waone kama jambo la Mungu ni swala la lazima. Hii ni hatari sana,hawa ni viongozi wetu wa kesho. Ni bora kuwa na taifa linaloongozwa na vichaa kuliko na viongozi wasiokuwa na hofu ya Mungu.
Kichaa hana laana,ila aliyemwacha Mungu anaitafuta laana. Kichaa huishi kwa neema za Mungu ila aliyemwacha Mungu huishi kwa laana za Mungu. Bora neema kuliko laana. Lakini kilicho bora zaidi ni baraka. Ambazo hupata yule aliyempendeza Mungu.
MWISHO.
Itapendeza sana kama hizi elimu zikawafikia na kuwaamsha usingizini. Asante.
DAVID M MROPE.
SUA.

Upvote
17