Ushauri kwa wanaotaka kuunga directly degree kutokea diploma mwaka huu.

HAZINA YETU

Senior Member
Joined
Mar 29, 2013
Posts
174
Reaction score
33
Naomba mtujuze wakuu namna ya kuunga degree moja kwa moja kwani namaliza diploma yangu mwaka huu na ningependa kuendelea na masomo ya degree mwaka huu mwezi wa kumi.

Kikubwa nahitaji zaidi kujua namna ya ku apply mkopo na TCU na ni muda gani natakiwa kuyafanya hayo ili kukimbizana na muda.

Pia mnijuze ada kiasi gani inahitajika kwa fomu za mkopo na TCU.
 
Tafuta chuo karibu na kwenu ili usev ila mkopo sahau labda kama ualimu wa sayansi au udaktari. Jipange babuuu
 
Heee... Ina maana mkopo ni kwa wale form six na diploma watakaosoma udaktari na ualimu wa Sayansi pekee ?
 
Wakati mwingine ndio maana huwa siikubali sana hii route ya kupitia diploma.Kwanza nafasi za kwenda degree huwa ni finyu( mfano out of 200 chances,only 10 ndio zipo for indirect entrants)

Mkopo pia huwa ni tatizo,except kwa afya na ualimu.Lakini pia basic courses huwa zinawasumbua kidogo inservices maana unakuta ni knowledge ya form six na wao wameshasahau

Kwa hiyo nadhani,mtu aende tu diploma kama alama zake sio nzuri sana kwenda degree moja kwa moja
 
Asikudanganye mtu mkopo kwa diploma upo palepale ili mradi una gpa not less than 2.7 utaomba kwa ku2mia sifa linganishi(equivalent qualifications) kwanza ukiomba nafasi ni rahisi kupata chuo kwa mtu mwenye diploma kuliko yule wa form six mwenye qualificatns za kawaida. Omba kaka na wala usiwaze njia nyeupeeee mkopo mpaka chuo.
 

Shukrani mkuu, aplication zinaanza mwezi wa ngapi? Ada za form ni kiasi gani?
 
Huwez pata mkopo labda utapata mdebe" we c umeunga unga elim yako basi na mkopo wr unga unga tu usome degree hiyo vinginevyo utasibir sana cku izi watoto wanaomaliza form six wanafaulu bana so huwez compet nao kwenye mikopo mkui
 
HESLB maombi ni april mwshon ada ni elfu 30+pesa ya kutumia kwa ems!halafu TCU hufungua kwenye mwezi wa sita au baada ya matokeo ya f6 na ada ni vocha yao ya elfu 50 inayouzwa bank ya NBC..cha msingi wakifungua omba ila tcu usubiri wakitoa guidebook itakayokusaidia kujua course utakazoomba!! achana na watu wanaokatisha tamaa kwani diploma huchukuliwa kama equivalent applicants na mkopo unapewa kama kawa kama tu course yako ni priority... kwa msaada zaidi ukihtaji ni pm
 

Hiyo heslb ni kwa ajili ya diploma peke yaka na ambao wanamaliza form six inakuwaje?
 
Mkopo huwezi pata Mkuu!! Coz wanafikirii wew tayar umeshaajiriwa ivyo unasalary! Uctegemee sana mkopo better uka-find another means.
 
higher education students loan board {heslb} ni kwa wote!! omba utapata
 
Shukrani mkuu, aplication zinaanza mwezi wa ngapi? Ada za form ni kiasi gani?
Application zimeanza tarehe: 02/ 04 /2015

Mwisho ya kufanya maombi ni tarehe: 18/ 07 /2015

Malipo ni: TSH 50'000/-

KUHUSU MKOPO:
Inategemea ni course gani wataka kusoma, Kuna baadhi ya kozi ukichaguliwa lazima ipate mkopo, Na baadhi ya cource ni bahati na sibu kupata au kukosa
 
Mkopo huwezi pata Mkuu!! Coz wanafikirii wew tayar umeshaajiriwa ivyo unasalary! Uctegemee sana mkopo better uka-find another means.

Namaliza mwaka huu halafu wahisi nimepata ajira kweli? Ngoja nijaribu mkuu.
 

Shukrani mkuu, nataka Laboratory technology kwani ndiyo nayomaliza nayo diploma. Vp nitapata?
 
mkopo upo kwa cozi za sayansi kasoro IT .haijalishi diploma au six ila uwe sayansi.kama ni art anza kutafuta panadol
 

Naona Watu wanageneratize Mambo sana Mkopo upo pale Pale kwa Wote.. ili mradi Sifa Za Mkopo unazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…