Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,047
- 1,832
Habari wakulima na wafugaji wenzangu, kumekuwa na malalamiko mwengi siku hizi kwa wakulima wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo cha papai kwamba wanakutana na mipapai dume mingi pindi wanaponunua miche ya mipapai kutoka kwa wazalishaji wa vitalu ya miche hiyo.
Siku hizi watu wamekuwa sio waaminifu, mtu anaweza kununua papai sokoni bila kujua aina ya mbegu akaja akaotesha miche kisha akaipachika jina lolote analojua yeye halafu akauzia watu, papai likishachakachuliwa mara nyingi lazima lipungue ubora na pia lazima upate mipapai dume mingi hata 50 kwa 50 kwani mbegu hybrid lazima ipatikane mbegu yenye sifa ya kike na ya kiume kwa hiyo kama itachakachuliwa sana inarudi kwenye sifa zake za awali.
NINI CHA KUFANYA?
Kama unataka kuwekeza kwenye kilimo cha papai na uwezo wako ni mdogo, nenda kwenye duka la pembejeo linaloeleweka nunua mbegu chotara inayojulikana hata ya Tsh 15,000 kisha otesha miche yako mwenyewe uitunze kwa uangalifu, ikishaanza kuzaa hapo unaweza kuchagua mipapai bora ukaotesha kitalu chako unachohitaji na idadi ya miche yoyote unayotaka. Hapo miche yako itakuwa ni bora kwani huo ni uzazi wa kwanza hivyo inakuwa haijapoteza ubora wake kwa kiasi kikubwa.
Kwa leo inatosha
Sent using Jamii Forums mobile app