Nelson Masaduki
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 346
- 380
Wanabodi,
Kama mlivyoshuhudia commitment ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuinua vipaji, kuwasaidia wanamichezo na wasanii hapa nchini, nawashauri Wasanii wetu wajitahidi kuiwakilisha Tanzania vizuri katika kila nafasi wanayopata. Tanzania inaendelea kukua zaidi na jina TANZANIA linaendelea kutangazwa vizuri na watu miongoni mwetu ambao wamebahatika kuwa na nafasi za kuwahudumia wanajamii. Ni matumaini yangu kuwa, endapo watajipanga vizuri, wanaweza hata kupata ardhi katika Jiji la Dodoma na kuliendeleza. Eneo hilo liwe na makazi mazuri ya wasanii ambayo yanaweza kutumiwa pia katika kurekodi filamu zao ama nyimbo zao. Mandhari ya eneo hilo ipangwe na wao wenyewe kwa kushirikiana na watalaam wa ardhi.
Kwa kufanya hivyo, watapunguza sana safari za kwenda kurekodi filamu ama nyimbo zao nje ya nchi.
Wanaweza kuwa na mandhari za aina mbili. Mandhari asilia na mandhari ya kisasa zaidi. Wasanii kama Mrisho Mpoto, wao mandhari zao si taabu sana kuzitengeneza na wanaweza kutumia mawazo ya Masoud Kipanya kama ilivyokuwa katika kazi yake ya Maisha Plus. Aliweza kubuni na kutengeneza vijiji ambavyo watoto wa mjini walikuwa wanakwenda kuishi na kufanya kazi kama vile wapo kijijini. Maeneo ya namna hiyo yanaweza kutusaidia kuwa na mazingira ambayo filamu, nyimbo na mambo mengine ya tamaduni zetu yakawa yanafanyika.
Mungu yabariki mawazo haya yatimizwe na wasanii wetu.
Nelson,
SUA-Morogoro
Kijiji cha Maisha Plus