Ushauri kwa Wazee wanaoanzia miaka 55 kuendelea

Mambo yote uliyoyaandika ni sahihi sana!
Mi nimeanza na kutafuta eneo nitakalozikwa,hivi sasa nipo nalifanyia fencing,humu ndimo nitakamopumzika mimi na uzao wangu wote!KUZIKWA HOLELA kwenye maeneo ya wengi ndiyo chanzo cha koo nyingi kuwa na mikosi!

Barikiwa Sana Mkuu
 
Mimi na miaka yangu 70 nimelipenda wasilisho lako mtoa mada. Asilimia 95 ya yaliyomo nayaafiki.
 
Andiko liko njema sana, kwa hio nijiandalie maziko yangu yawe huku huku kwa Trump sasa. Mambo ya sijui nikazikwe bongo, Naaah.
 
Miaka 55 sio Mzee bali mtu MZIMA. Uzee unaanzia miaka 65.

Miaka 60 tunasema sasa umevuka angle ya utuuzima unaenda kuzeeka. Ndio maana Hata Utumishi , kustaafu ni 60 years, from there

Umewakosea heshima watu wazima wa 55 kuwaita wazee

By the way ulichoandika ni irrelevant na hali halisi, kwa sasa tunavijana wa 35 years old - ana diabete , High BP, Osteoporosis, ana undergo physiotherapy ya Mgongo na mifupa, ….a lot of them
Vijana wa 30s tayari wanalalamika kiuno na migongo vinauma. As a Medical Profession, I speak by Experience.

Unakutana na hao unaowaita wazee hana kisukari hana presha havai glasses , fit and hana ishu za migongo..

Kuhusu upweke vijana wa 25 are lonely na ni wapweke sana..::: wengine ndio hao wanajiangusha kwenye magorofa……

Uchawa wa vijana kwenye siasa ni aina nyingine ya Upweke na defeat ya wazee dhidi ya vijana.


In his 40s Obama aliaminiwa na kuwa Rais. Huko TZ kijana wa 40s ni bado mtoto lol

Hayo mengine uliyoandika kama Chupi ni cut cross kwa rika zote na inategemea Mila desturi na utamaduni wa jamii

Otherwise 55 ndio Umri wa Highest level of maturity kwa vijana….. na kama una good life style ….. utaonekana bado mtoto
 
Umemaliza,Mimi April ndio nimefikisha 55, Lakini Kuna Jamaa yangu ana 48Yeye anaamkiwa Shikamoo,Mimi naambiwa vipi bro!Hii Inategemea na Tabia ya kula, mazingira nk!
 
Nina miaka 78. Yote uliyoandika yana mashiko japo mengi ni common sense tu.

Wakati na nyie vijana mkiserebuka kuna jambo moja naomba mlikumbuke sana. Miaka itakimbia sana hapa katikati na ukija kushituka utajikuta uko 40s tayari. Tunzeni na kulinda sana afya zenu kuliko cho chote mlindacho. Angalia ulaji wako. Angalia uzito wako. Pombe. Sigara. Ngono zembe; na tabia zingine zote hatarishi zinazoweza kuhatarisha afya yako.

Fanya kila lililo ndani ya uwezo wako ili kuhakikisha kwamba unaingia huku 60s na 70s ukiwa huna magonjwa sugu. Ukikamata kisukari, presha, magonjwa ya moyo; na mengineyo aisee hakuna rangi ambayo utaacha kuona hata kama una vihela vyako; na kamwe hutakaa ufurahie uzee wako.

Ni hilo tu kwa sasa! 🙏🏿

 

Shukrani Sana Mkuu.
Kwa niaba ya vijana tumepokea ushauri wako
 
Nafikiri mleta uzi amewatarget wazee wa bongo maana kibongo bongo ukiwa na 55 wanaona umezeeka na ndio maana wanastaafu wakifika 60. Kwa mamtoni huku ukiwa na kwenye 50 - 55 bado wanakuita "young boy" hadi ukiingia 60 - 65 hivi, na hii nadhani inatokana na life span. Africa kizazi hiki cha sasa kukatiza 50 ni mbinde sana shauri ya haya mavyakula na huduma za afya zilizo duni.
Anyway, mleta uzi ana point nyingi za msingi kwa wanaokaribia dakika za majeruhi.
 

Kibongobongo familia nyingi hazina hao watu wenye Miaka 60. Hivyo wazee. Wao huanzia 55 huko.

Ingawaje ulichosema ni sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…