Ushauri kwa Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo

Ushauri kwa Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo

Queen Esther

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,206
Reaction score
1,464
Waziri Kijana Mhe. Selemani Jafo nimekusoma kuhusu taarifa ya kuwaondoa Wakurugenzi waliopata hati chafu.

Nakupongeza kwa uamuzi huo ingawa naomba kukushauri yafuatayo:-

1. Kuna Majiji, Manispaa au Halmashauri zimepata hati safi sababu ya kutoa rushwa kwa timu ya CAG!!! Tafadhali chunguza hili!!! Wapo waliopata hati chafu sababu walikataa kutoa rushwa, wapo waliofanya madudu zaidi yao na wana hati safi.

2. Kwenye Mashirika ya Umma huko ndiko balaaa. Rushwa kwa timu ya watu wa CAG inatolewa yakutishaaa! Ndio maana kuna mashirika yanatisha kwa ufisadi wa miradi, huduma mbaya kama za wastaafu nk na bado wamepata hati safiii!

Ni wakati wa kufanya kazi nje ya box!! Au kuondoa kabisa box!

Hongera Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan. Naiona Tanzania ikipiga kasi ya maendeleo ya ajabu kabisa.
 
Duuu uki vizuri mkuu ungeweka na mfano wa halmashauri husika ingependeza sana
 
Una maanisha CAG naye anafaa kuchunguzwa na TAKUKURU kwa kupokea hongo na kugawa hati safi kwa wasio stahili?
 
Siku zote umekuwa ukituambia hapa JF kuwa serikali ya Magufuli amefanikiwa kuondoa kabisa rushwa kwenye taasisi za umma, sasa hii inakuwaje?

Yaani juzi tu Magufuli amezikwa leo umebadilika na kusema serikali ya Magufuli ilikuwa imejaa rushwa kupindukia!!

Kweli umetisha.
CCM na unafiki ni kama pete na kidole.
 
Baada ya Magufuli akili zimeaanza kuwakaa eeeh!
Wote sasa tunaimba wimbo mmoja wa kusema serikali iliyopita ilikuwa ni serikali ya wala rushwa kupitiliza!

Kweli marehemu hana lake.
 
Ni kweli wafanyakazi wa CAG wanachukua rushwa ili watoe hati safi. Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom