Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Naomba nitoe ushauri kutokana na tetesi nilizosikia, nitashukuru kama nitaeleweshwa iwapo ushauri wangu si mwafaka. Lakini pia naomba nisirushiwe maneno yenye kuudhi kutokana na ushauri wangu, nikielimishwa "itapendeza zaidi"
Jana jioni nilikuwa safarini natokea Dodoma kuja Mikumi, nilipofika eneo la Dakawa karibu na njiapanda ya kwenda kiwanda kipya cha sukari Magereza kama sijakosea, nikaona kuna miti inaangushwa kwa wingi, nikawauliza abiria wenzangu kulikoni, wakasema serikali inajenca chuo cha ualimu, lakini abiria mmoja akaanusha na kusema eneo hilo linaandaliwa kwa ajili ya kujenga mizani nyingine baada ya ile ya Morogoro mjini kutokuwa katika eneo sahihi.
Pendekezo langu kama ni kweli Mizani ya Morogoro inahamishiwa Dakawa kutokana na sababu mbalimbali za kitaalamu, basi nami ningependekeza mizani hiyo ingejengwa eneo la Sokoine. Hii ninadhani itasaidia sana kupunguza uharibifu wa barabara kwa kipande cha kilomita 50 kuanzia mji wa Dakawa na Morogoro mjini kutokana na sababu kwamba magari mengi yatapakia mzigo mwingi zaidi kutoka eneo hilo la Dakawa kuelekea Morogoro mjini kwakuwa hakutakuwa na mizani yoyote inayodhibiti uzito wa magari yatakayopakiwa mchele kutoka eneo hilo hadi Morogoro mjini, ikumbukwe kwamba eneo hilo la Dakawa linazalisha mpunga kwa wingi sana ambao hukobolewa na kuwa mchele katika eneo hilihilo.
Huo ni mtazamo wangu, naomba kuwasilisha,