Kwa mfumo wa elimu ya nchi yetu Tanzania (sijui nyingine) ni wazi kwamba tunasoma kwa muda mrefu mambo mengi yasiyohusiana ma taaluma tunazozipenda kutoka shule za msingi mpaka kidato cha sita kwa mfano: kutoka darasa la kwanza mpaka la saba tunasoma ili tufaulu mitihani tu, kidato cha kwanza na pili kinaamua kidato cha tatu na nne usome arts au sayansi ili kufaulu mtihani kidato cha nne.
Matokeo kidato cha nne yanaamua nani aende wapi na asome nini kama vile ualimu cheti, nursing au kidato cha tano na kuanzia hapa tunaanza kupata watu wenye taaluma fake kama waalimu na manesi. Wengi wa watu waliomaliza kidato cha sita hawajui wasome kozi gani chuo kikuu, je kwa mfumo huu tunapata wataalamu kweli au wataalamu bandia!??
Hii ndio sababu kubwa vijana wengi wanabaki mitaani na kukosa ajira pindi wanapomaliza elimu zao kwa sababu yote waliyosoma walichaguliwa na mfumo uliopo na walioajiriwa wanaleta matokeo mabovu ya kazi kwa kukosa ubunifu kwa sababu walivyosomea sivyo walivyovipenda.
USHAURI WANGU Kwa wale wanaojiunga na vyuo mbalimbali, mjitahidi kuchagua kozi mnazozipenda na sio mnazoshinikizwa kusoma kwa sababu hayo ni maisha yenu na wanaowashinikiza hawatawasaidia pindi mkimaliza na kupata shida na kitu unachokipenda ni rahisi kukitafutia ajira ya kujiajiri au kuajiliwa.
Ili nchi hii iendelee ni lazima tupate wataalamu sahihi na nyie ndo wadau wakubwa. Watu wanaokuzunguka wanatakiwa kuwa washauri na sio waamuzi wako na usikilize na kuchambua ushauri wao kwa makini kabla ya maamuzi. Ni hayo tu ndugu zangu na nawaombea msome vitu mnavyopenda tupate wataalamu
wa kweli na sio wa kubabaisha babaisha (wajanja wajanja).