USHAURI:kwenda kusoma masters au kujikita kwenye biashara/ujasiriamali kipi bora?

USHAURI:kwenda kusoma masters au kujikita kwenye biashara/ujasiriamali kipi bora?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Habari,Wadau mimi ni mwalimu nina bachelor ya education,nimejichanga nimepata vijisenti kama m.5 na ushehe,nikiangalia changamoto za ualimu napata hasira sana natamani niende nikasome shahada ya pili tofauti na kozi za ualimu but napata wakati mgumu ni kozi ipi nisome?

kwa upande wa pili nakumbuka kuajiriwa ni utumwa ni bora kupambana na maisha kwa kujiajiri kwani m.5 zinatosha kwa mtaji,ila hapa napata ugumu pia mradi gani unanifaa,niko very interested biashara na kufuga ila kikwazo ni upatikanaji wa maeneo kwani kwa huku niliko(lushoto) jiografia yake ni mbaya milima kiasi kwamba ardhi imekua ghali na adimu sana japokua kuna stawi mazao mengi ya chakula na biashara kutokana na hali nzuri ya hewa na mvua za uhakika.

KEBEHI NA DHIHAKA WEKENI KANDO KAMA HAUNA CHA KUCHANGIA NI BORA UKAPITA TU.

# BARAKA ZIWE NANYI#
 
ushauri wangu ni huu, angalia mapato yako je yanakuridhisha na unajiona wapi baada ya miaka 10 au 20 kwa hiyo kazi au biashara unayotaka. Naona umetaja kusomea profession ingine kama first option halafu biashara kama last option. Kipi hasa kipo moyoni mwako? kama wewe unapenda ajira ila tu unaona ualimu ni mbaya basi nenda tu kasome utafute kazi ingine siku hizi vyuo vingi au hata uende wizarani kwa kazi kama wakaguzi nk. Biashara au ujasiriamali inabidi uipende kwanza maana changamoto ni nyingi na ni vita ya mtu mmoja sio tena kuwa chama cha sijui walimu au wafanyakazi wakutetee huko ni wewe mwenyewe na competition ni kubwa. kwa kuanzia soma mabandiko mbalimbali ya ujasiriamali hapa na uone kama unaweza pia somo mabandiko jukwaa la elimu kwa kozi mbalimbali. Kila la heri
 
Habari,Wadau mimi ni mwalimu nina bachelor ya education,nimejichanga nimepata vijisenti kama m.5 na ushehe,nikiangalia changamoto za ualimu napata hasira sana natamani niende nikasome shahada ya pili tofauti na kozi za ualimu but napata wakati mgumu ni kozi ipi nisome?

kwa upande wa pili nakumbuka kuajiriwa ni utumwa ni bora kupambana na maisha kwa kujiajiri kwani m.5 zinatosha kwa mtaji,ila hapa napata ugumu pia mradi gani unanifaa,niko very interested biashara na kufuga ila kikwazo ni upatikanaji wa maeneo kwani kwa huku niliko(lushoto) jiografia yake ni mbaya milima kiasi kwamba ardhi imekua ghali na adimu sana japokua kuna stawi mazao mengi ya chakula na biashara kutokana na hali nzuri ya hewa na mvua za uhakika.

KEBEHI NA DHIHAKA WEKENI KANDO KAMA HAUNA CHA KUCHANGIA NI BORA UKAPITA TU.

# BARAKA ZIWE NANYI#

Unataka ukaongeze elimu ili mchahara upande na cheo?????

naamini ukienda shule hutakuwa na amani.....kwani hiyo pesa haitoshi........naweza nkaopnge mengi ila msikilizae huyu mzee na umuelewe........fanyia kazi utakachojifunza.....usisahau kuja kutupa feedback

Movers and Shakers: Muguku - YouTube
 
Ualim mshahara unapanda kwa uzoefu wako sio elim! Kuna walim wa cheti wakongwe wanaenda sawa na degree asiye na uzoefu
 
Ualim mshahara unapanda kwa uzoefu wako sio elim! Kuna walim wa cheti wakongwe wanaenda sawa na degree asiye na uzoefu
Je umeshajiuliza huyo wa degree akija kukaaa kazini kwa muda kama wa mwalimu huyo ya cheti atakuwa na mshahara kiasi gani? Najua jibu litakuwa bado elimu inaleta utofauti, maana unaweza kuta mtu wa degree anapata mshahara sawa na mtu wacheti aliye kaa kazini zaidi hata ya 10yrs. Pia ujue kuwa katika kupanda kwa madaraja serikalini kuna ukomo wa kupanda kulingana na elimu. pia hapo ndio gap linapoaanzia ni kweli ulitangulia ila umefika mwisho mwenzio anakufikia na kukuacha hapo mpaka unastaafu.
 
Mkuu kwaupande wangu bora biashara
ili uachane na kazi za watu pia upate nafasi
nzuri ya kujituma wewe mwenyewe kuliko
kutumwa.

Kwasasa hali ya maisha ni mbaya pi mshahara
pekee hautoshi kitu chochote.
Kila la heri kwenye biashara Mkuu wangu.
 
Mkuu,Lushoto ni moja ya sehem ambazo kuna fursa nyingi za kibiashara Unaeza ukabaki kwenye kazi yako halafu ukawa unanua mazao,unafuga na kuanzisha hata duka lako Mimi naitamani sana iyo Mil.5 aseee
 
Ualim mshahara unapanda kwa uzoefu wako sio elim! Kuna walim wa cheti wakongwe wanaenda sawa na degree asiye na uzoefu

Amesema anataka kusomea field tofauti pengine anataka kubadili career pia.
 
Miaka hii siyo ya kukaa kazini ukiongojea upande daraja na kiwango cha mshahara. Fanya kazi ukiwa na malengo dhabiti ya kuhakikisha unastaafu kwa hiari yako baada ya kujiimarisha kibiashara.

Kuajiriwa iwe ni ngazi ya kukufanya ujiajiri mwenyewe.

Mkuu nakushauri ufanye utafiti wa kutosha uanze biashara, na kwa ualimu huu nao ujua una muda mwingi sana wa kufuatilia biashara zako.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Uamuzi wa Mtu kwenda Kusoma au Kuingia katika Biashara ni wa mtu binafisi, ni lazima wewe mwenyewe uangalie ni wapi unataka kustick na ulicheki na feature yako ya baadae unataka kuwa nani.

Kila kitu kina ugumua wake, kwenye maters unaweza soma ukaliwa kichwa kabla ya kuhitimu, the same katika biashara, kuna changamoto za kufa mtu, ambazo usipo kuwa na spirit ya uvumilivu unaweza kimbia mapema n kurudi kufundisha, hivyo ni lazima wewe mwenyewe uchukue uamuzi sahihi,

Kama ni Biasara maana yake unajiandaa KCHOMA MELI MOTO,
 
Back
Top Bottom