Nawapongeza wasafi kwa jitihada za kuwaleta kina medd, wizkid na tiwa savage katika tamasha la wasafi ila kama ilivyo kawaida wahudhuriaji wa show wamebaki tu kushangaa shangaa ni nini kinaendelea uwanja ukiwa umepoa sana bila shangwe.
Sidhani kama wamepokelewa kama walivyodhani kwa sababu wahudhuriaji wameonekana kutojua chochote kinachoimbwa kwa kiingereza ambacho wengi kimewapita kushoto.
Si hawa tu bali hata kina rick ross, jay z, n.k waliwahi kuja fiesta watu wakabaki wanashangaa shangaa tu.
Ni ushauri tu kwamba aina hii ya wasanii wana gharama kubwa kukodishwa ila wakifika hapa ni heri angelipwa hata man fongo kupafomu hainaga ushemeji ].\\\[[[[