Ushauri: Kwetu hawamtaki mwanamke niliyezaa naye mtoto

Jayselejm

New Member
Joined
Feb 22, 2023
Posts
3
Reaction score
12
Mimi nina mwanamke kiukweli nampenda sana na yeye ananipenda na tumejaaliwa kupata mtoto mdogo wa kike, lakini nyumbani kwetu hawamtaki hasa mama yangu mzazi pamoja na dada zangu.

Ukizingatia mama yangu ananipa sapoti kubwa na mambo mengi amenitendea kunilea, kunisomesha kuanzia shule ya msingi mpaka kupata degree na hata sasa ni msaada mkubwa kwangu.

Wakuu karibuni
 
Dogo acha ufalaa ... Msikilize mama yako
 
Ogopa kufanyiwa maamuzi na wazazi au ndugu, simama kama mwanaume, mwisho wa siku watakufuata.
 
Sababu zinazowafanya wasimtake ni zipi? Pia je wewe unaona huyo binti ana mwenendo mzuri? Usikute ana mwenendo mbaya ndio maana ndugu wanakwambia ukae mbali ila wewe mahaba yanakuzuzua unataka uingie hapo.

Tupe sababu za mama na dada kumkataa huyo mwanamke.
 
Sababu kuwa wanadai hana maadili kutokana na mavazi anayovaa,pmj na familia yao inashida lkn mim naona ni kwakuwa bado mdg mamb hayo ya mavaz ataacha tu cz nmeshaongea nae kuhusu hilo
 
Sababu kuwa wanadai hana maadili kutokana na mavazi anayovaa,pmj na familia yao inashida lkn mim naona ni kwakuwa bado mdg mamb hayo ya mavaz ataacha tu cz nmeshaongea nae kuhusu hilo
Ataacha au kaacha?
 
Sababu kuwa wanadai hana maadili kutokana na mavazi anayovaa,pmj na familia yao inashida lkn mim naona ni kwakuwa bado mdg mamb hayo ya mavaz ataacha tu cz nmeshaongea nae kuhusu hilo
Ila mitoto ya siku hizi bwana eh. Kwa hiyo,ulivyoona mipaja nje nje,ukaona umeoa! Ulichofanya ni uzinzi. Wangemkataa kisaa mfupi,masikini,...... ningekushauli ukaze roho. Ila kitendo cha kuonekana hana maadili,inaonyesha wazi mzazi alivyokuhangaikia,na wewe ulivyomuangusha. Hapo tayari umeanza kutengeneza kizazi cha shido. Mama hapendwi,yaonekana ulishakua mhuni, huyo mtoto unadhani mwisho itakuwaje?
 
Mi naona umempeleka mbali sana ni kama unamuambia ajitenge na familia yake na ategemee zaidi marafiki na makundi mapya,nadhani hii SIO SAWA. Tafadhali kijana mleta mada pata utulivu jua sababu ya kwanini mzazi hamtaki mwenzako.Wazazi wana uzoefu wa mambo ya mapenzi kumbuka,pia maisha ya unyumba.Ukiwa kijana kuna vitu unaweza usivione lakini wazazi wanaona.Hivyo penda kujua sababu na ongea na mzazi kwa upendo uweke msimamo wako(kama unavyoona) na mmalizane na mzazi kwa amani; hata kama ni kukubaliana kutokubaliana.
Kumbuka familia yako ni kitu bora sana na hata dunia ikikutenda familia yako(hasa wazazi na hasa mama) ndio watasimama nawe hadi mwisho.
 
Sababu kuwa wanadai hana maadili kutokana na mavazi anayovaa,pmj na familia yao inashida lkn mim naona ni kwakuwa bado mdg mamb hayo ya mavaz ataacha tu cz nmeshaongea nae kuhusu hilo
Kwanini unaoa mtoto mdogo??
Kama hilo la mavazi ya kuzingatia ukweni kashindwa ataweza kukusikiliza kwenye mambo mtambuka ya ndoa??
Usipokuwepo yeye anaweza kua mbadala wako hata hapo kwenu??

Bila shaka hata wewe ni mdogo kama yeye, fikiri mara mbili kijana, hilo kukimbilia kumtia mimba binti mdogo ni kosa.
 
Hivi kweli unajua na degree bado unapata masaada kwa maza maza na Dada zako wamekuona wewe ni mzigo alafu unataka kuwaongezea mizigo isio na tija?dah elimu nilijua ungesema wewe sasa baada ya kusomeshwa hiyo family ndio unaisapoti
 
Mbona kama bado hujakua?
 
Hivi unaanzaje kumpenda mtu. eti ananipenda nami nampenda . upuuzi mtupu
matumizi mabaya ya upendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…