Ushauri maoni juu ya malipo ya NSSF

Ushauri maoni juu ya malipo ya NSSF

bolivia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2021
Posts
3,083
Reaction score
5,179
Hbr na poleni na swaum wana JF:-

Niende kwenye point kuu ya mada hii nina mzee wangu anakaribia kustaafu serikalini kama mtumishi wa umma kwenye kada ya afya, tumezaliwa watoto 4 Mungu ni mwema wote tulibahatika kwenda na sasa tumebahatika kwa uwezo wa Mungu tupo kwenye ajira nini pointi yangu ya kuleta hii thread hapa jukwaani??

Anayestaafu ni mzazi wangu lkn mimi kama mtoto wake mkubwa sio mbaya nikawa na kitu cha kumshauri kwa mafao yake na mapumzko yake baada ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu sana maana nina meeting nae next week ndani ya mwezi huu wa 4

Nafaham zile hela zao zinakujaga nyingi kwa mkupuo ili asiweze kuteleza kama wastaafu wengine maoni yako kama mdau kama ndugu au rafiki ktk Jamii Forums na uzoefu wako juu ya haya masuala ni vitu gani naweza mshauri mzee wangu vya kufanya baada ya kupokea haki zake ili asiweze kutetereka kiuchumi baadae maana ni pesa ambayo inatoka tu bila kuingia

Kwako mwanaJF

Natanguliza shukrani. Karibu.
 
Hiyo hela ni kwa ajili ya ku-repair mwili wake, na kupata mahitaji muhimu tu pale dharura itakapotokea; sio hela ya kufungua biashara wala kununua mifuko ya simenti au tofari. Naamini mpaka kufikia umri huo, atakuwa alishajipanga vya kutosha.
 
Ni Bora akawekeza kwenye Bond za serikali- awe anakula interest kidogo kidogo, na mtaji uko pale pale- kwa mstaafu ni uwekezaji mzuri kuliko biashara au kuweka tu pesa na kutumia
 
Ndugu yangu, kua makini sana unapoenda kushauriana nae. Wazee wengi hua hawajawahi kushika kiasi kikubwa hivo cha pesa maisha yao yote, so wakiipata ni kma wanachanganyikiwa. Kua makini na ushauri utakaompa maana in any way ukibuma anakulaani. Kama akipewa hyo hela mwambie 75% aweke benki tena fixed japo miez 6, af ingine aanze kuichoma ili azoee.
Bahati mbaya hua hawasikilizi utadhani watakufa kesho
 
kuna mwalimu mmoja mwaka 2015 alilipwa pension yake akatoroka na house girl wake mpaka leo hajarudi wala kurudishwa kwa mkewe

#chuchu saa 6
 
kuna mwalimu mmoja mwaka 2015 alilipwa pension yake akatoroka na house girl wake mpaka leo hajarudi wala kurudishwa kwa mkewe

#chuchu saa 6
Aaah aaah
 
Back
Top Bottom