Wakuu habari,
Nina mshkaji wangu yupo Morogoro, wana kesi walishtakiwa ya kiofisi Tangu mwaka 201, upande wa Jamhuri walileta shahidi mmoja tu, ishapita miezi hawajaleta shahidi mwingine, Sasa ananiambia mwezi uliopita Hakimu alitaka kuwafutia kesi maana kashaichoka na ni ya muda mrefu Sana.
Sasa bwana anasema upande Jamhuri waliwaandaa polisi hili wakiachiwa tu wakamatwe Tena, na anasema wakikamatwa tena kesi nasikia inaanza upya na kwa Hakimu mwingine, na masharti mapya ya dhamana.
Hii inakaaje kisheria, mbona sheria zetu kama ni hivyo ni za ovyo sana na kiuonevu kwa raia wake.