Shahada za kitanzania hazina soko hata kwenye jumuia ya afrika mashariki kwenyewe. Ukienda ulaya ndiyo usiseme. Lazima wakutupe darasani hasa chuo chenyewe kama ni vile vinavyoheshimika. Wazungu wanajua elimu yetu ilivyochakachuliwa na ufisadi. Kwa Open University ukweli ni kwamba wengi wamejenga dhana kuwa ni chuo ima cha wanasiasa aina ya akina Mrema au watu waliofeli au wenye tamaa ya kuwa na shahada mradi shahada. Leo nimeshangaa kusoma makala ya mtu mmoja aitwaye Hamza KONDO eti mwanafunzi wa PhD na mhadhiri OUT. Jamaa hajui hata kuandika makala kwa kiswahili. Hivi mtu kama huyu kweli anaweza kuandika academic paper au dissertation?