ushauri matokeo yangu mabaya( div zero)

ushauri matokeo yangu mabaya( div zero)

Wij

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
478
Reaction score
142
jamani nimepata F zote yaani nna zero ya 21 nifanyeje? Nilikuwa nachukua HKL
 
Form 4 ULIPATAJE?? COZ HAPO HAUNA JINS LAZIMA UTUMIE YA 4M 4 AU KA VP RESEAT
 
Tumia cheti cha form 4 kama ni kizuri nenda certificate courses kwa hkl nenda ya social work
 
Matokeo yako ya F. IV yalikuwaje? Na unataka kuwa nani hapo baadaye?
 
form four nilikuwa na IV 26
 
jamani nimepata F zote yaani nna zero ya 21 nifanyeje? Nilikuwa nachukua HKL

Tuambie kwanza wewe una mpango gani/ unapenda nini? tusije tukawa tunakuchagulia hatma ya maisha yako bila ridhaa yako.
 
Kuna extenuating circumstances ambazo zimekufanya upate zero?
Otherwise, unaweza kushauriwa urudie au usome kitu kingine na bado ukafeli tena.
 
form 4 div 4 form 6 div 0, haya bana. ila pole, coz shule ni part ndogo tu katika mafanikio maishani, mradi umeondoa ujinga, sasa ni jitihada zako kama bado unatamani mafanikio kupitia kalamu, either uendelee na shule, au utafute maisha.
 
Kama utaamua kusoma fani yoyote ngazi ya cheti; hakikisha una uhakika wa kazi. Kuna rafiki zangu wengi waliopata Div IV O-level; waamua; wengine kwnda uplisi, kufanya biashara, askari magereza, driving n.k Kwa sasa wana utajiri mkubwa + familia. Mimi bado nasongoka na test, semina, presentation n.k. Kufanikiwa maishani hakutegei elimu ya darasani bali BUSARA, UBUNIFU NA ELIMU YA MTAANI(street wisdom)
Pia, kama unaweza kufanya kazi za kujiajiri ni vyema sana.
Sikushauri sana kurudia shule....
KUFANIKIWA NI LAZIMA, BILA HATA YA KUWA NA ELIMU YA CHUO KIKUU
 
kulingana na matokeo yako ya form four mkuu kichwa chako sio cha darasani... tafuta mradi fanya biashara...
 
Kuna mambo mawili yanayokufaa kwa uwezo wa akili yako, 1) ufugaji 2) kilimo. ukijitoa mhanga katika vitu hivyo viwili kwa muda wa miaka 2 kwa resources zilezile ambazo ulizitumia kusoma f5&6 utapata majibu tofauti na division zero. fanya ufugaji wa wanyama wasiohitaji mtaji mkubwa, wasiohitaji processed products n.k
 
kakaa,du,maneno makali sana hayo punguza munkari,mshauri dogo usimponde,yupo kwenye hard time but me nimempenda ni muwazi sana,lazima atoke kimaisha huyu hata kama kafeli shule
 
Back
Top Bottom