Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kuna baadhi ya tabia hupaswa kufuatwa ili afya ya kinywa na meno iweze kubaki imara siku zote.
Kwa mujibu wa Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC), haya ndiyo mambo ya msingi kuzingatia unapokuwa unatumia mswaki wako.
Chanzo: CDC
Kwa mujibu wa Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC), haya ndiyo mambo ya msingi kuzingatia unapokuwa unatumia mswaki wako.
- Unashauriwa kubadili mswaki wako kila baada ya miezi 3-4, au muda wowote ule kabla ya hapo ikiwa tu utahisi kuwa ubora wake umepungua. Miswaki iliyopungua ubora wake hupunguza ufanisi wa kazi.
- Usifunike mswaki wako kwenye chombo chochote baada ya kuutumia. Kitendo hiki husababisha kuzaliana kwa bakteria.
- Hauhitaji kutakasa mswaki wako kwa sanitizer, spirit, kemikali zozote kali au kwa kutumia mionzi ili kuua bakteria wake. Vitendo hivi siyo salama kwa afya ya mtumiaji.
- Safisha mswaki wako kwa maji tiririka, kisha uhifadhi kwa kuusimanisha. Kama sehemu husika ina zaidi ya mswaki mmoja, hakikisha haigusani.
- Mswaki unaweza kusabambaza magonjwa. Hata kama ni ndugu, au mnapendana kiasi gani, kila mtu atumie mswaki wake.
Chanzo: CDC