Ushauri: Matumizi sahihi ya Mswaki

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kuna baadhi ya tabia hupaswa kufuatwa ili afya ya kinywa na meno iweze kubaki imara siku zote.



Kwa mujibu wa Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC), haya ndiyo mambo ya msingi kuzingatia unapokuwa unatumia mswaki wako.
  • Unashauriwa kubadili mswaki wako kila baada ya miezi 3-4, au muda wowote ule kabla ya hapo ikiwa tu utahisi kuwa ubora wake umepungua. Miswaki iliyopungua ubora wake hupunguza ufanisi wa kazi.
  • Usifunike mswaki wako kwenye chombo chochote baada ya kuutumia. Kitendo hiki husababisha kuzaliana kwa bakteria.
  • Hauhitaji kutakasa mswaki wako kwa sanitizer, spirit, kemikali zozote kali au kwa kutumia mionzi ili kuua bakteria wake. Vitendo hivi siyo salama kwa afya ya mtumiaji.
  • Safisha mswaki wako kwa maji tiririka, kisha uhifadhi kwa kuusimanisha. Kama sehemu husika ina zaidi ya mswaki mmoja, hakikisha haigusani.
  • Mswaki unaweza kusabambaza magonjwa. Hata kama ni ndugu, au mnapendana kiasi gani, kila mtu atumie mswaki wake.

Chanzo: CDC
 
Asante sana kwa taarifa..

Ila inashangaza wapendanao wasitumie mswaki mmoja ila French kiss ruksa.

Anyway tutunze afya ya vinywa vyetu kwa kusafisha si chini ya mara 2 kwa siku...kwakutumia mswaki na dawa nzuri ya meno.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…