Nina eneo lenye ukubwa ya karibia nusu heka maeneo ya Kimara Suka, Kama dakika tano toka Morogoro road kwa mguu. Kuna mjengo ambao haujaisha, ambao unaweza kuwa hall ya sherehe, godown, ama office. (kupangisha bank, kampuni ya simu, nk). Kwa hivyo vitatu hapo ipi italipa zaidi, kuna utaratibu gani wakupangisha bank ama ATM zao.
KULIPA wamaanisha kitu gani, kuwa biashara izo unaziendesha wewe au we chako ni jengo unataka kukodisha tu ambapo kodi yako haibadiliki kulingana na bei ya soko lilivyo mahali hapo? Tunaomba ufafanuzi nachofahamu mie bei ya pango haitegemei aina ya biashara ila hadhi yake na soko la upangishaji wa mahali husika.