Ushauri: Michirizi inamsumbua mama watoto, afanye nini iache kumuwasha?

Ushauri: Michirizi inamsumbua mama watoto, afanye nini iache kumuwasha?

fundi bishoo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2018
Posts
14,264
Reaction score
27,132
Habari zenyu kwema?

Bwana mwaka huu mama watoto wangu ametokwa na michirizi baada ya kutumia losheni ambayo alikua hatumii mwanzo, inaitwa sitii sijui baada ya kutumia hajamaliza hata wiki 2.

Wiki moja haijapita zikamtoa michirizi kidogo akaacha kabisa kupaka, sasa ajabu inakua inamuwasha na inaongezeka kila anapokuna. Je, kuna namna inaweza kusaidia ikaacha hata kumuwasha maana anapata tabu si mchezo?

Msaada wenu kwa wabobezi afanye nini ili tu isiwashe maana naskia michrizi haitokag ikikupata imekupata.
 
Ct ni bomu mkuu mwambie aachane nayo atafute bio oil awe anapaka mkuu yawe ndio mafuta yake hiyo michirizi itaenda itapungua na aachane na lotion yoyote kwa sasa kitendo cha kupaka lotion tu michirizi inazidi
 
Back
Top Bottom