Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

Bora ukaanza biashara kidogo kidogo ukiwa unaendelea na ajira, maendeleo ya biashara yako ndiyo yakulazimishe kuacha kazi, labda kama biashara hiyo ulishaifanya unaijua.
good point, lakini yy ameamua kuwa risk taker
 
Si utapeli kwani anachukua mafao yake kwa mlango wa nyuma
Hapo sasa lazima acheze deal na mwajiri maana bank wamekuwa wajanja sana siku hizi .....kwanza kama una contract ya mwaka mwaka mkopo unakuwa mgumu kweli na ndio maana wanataka committment ya mwajiri...unless ufanye kosa la makusudi mwajiri akupige chini ukiwa ndani ya mkopo ili baadae mkae chini kuweka sawa mambo
 
Miaka ya nyuma tumefanya sana ivyo namm nilifanyaga zaidi na Mara nyingi, tulikuwa salama na tupo salama ila kwa miaka hii jambo hilo ni gumu sana. Ili upate mkopo NMB kwa mfano lazima pamoja na kudhaminiwa na mwajiri upate mdhamini mwingine ambaye ni mfanyakazi wa serikali kwa iyo uki default wanamfata mwenzako.
 
Hakuna haja ya ninyi watoa ushauri kurumbana. nadhani jambo la busara ni kutoa ushauri kwa muomba ushauri na kisha tumuachie yeye afanye Maamuzi. kwa sababu Mwanaume anachanganya za kwake na za kuambiwa
 
Mkuu naona ushauri wako ni mzuri ila kama technical sana (wa kisheria). Ila kama mimi nachangia kwenye mfuko wa kijamii, halafu nataka Kuacha kazi lakini wanagoma kunipa fao la kujitoa kwanini nisikope halafu deni langu litajilipa juu kwa juu
 
Wakuu..
Nimepitia comments zenu zote naona wengi mnakurupuka kunipa ushauri bila kusoma Maelezo yangu....

Mnasema nisiache Kazi, niendelee na hiyo business yangu mdogo mdogo. Kumbukeni nimewaambia kuwa Kazi ndio inanifanya nikose muda wa Kudeal na business yangu. Ndio maana nataka niache Kazi.

Mara mnasema nidundulize kidogo kidogo.
Mnajua kuwa muda ni Mali. Hiyo opportunity nishaifanyia intensive analysis. Najua potential profit na loss zake.
Changamoto ni Time and capital.

Suala langu lilikua nikikopa pesa kisha nikaacha ajira inawezekana???
Suala la kuwa ni kosa, sijui sio ustaarabu namie najua.
 
Ndugu yangu kama kweli unataka kukopa million 5, halafu ukimbie nchi, ni pesa ndogo sana, hutafika mbali. Vyuma bado vimekaza ila sikushauri kwa hilo
 

Jamani huu siyo wizi.....inategemea na mkataba wako wa ajira unasemaje...hata kwenye fomu ya mkopo inaeleza bayana kwamba ikitokea mwajiriwa amefukuzwa au ameacha kazi basi bank iitapataje hela yake kupitia mwajiri
 
Saa hii wewe unatakiwa uwe kwenye lockup za polisi kwa kosa la kutaka kufanya uhalifu,
 
Mkuu chukua tuu mkopo na uanzishe hyo bussesnss unayowaza bt USIACHE KAZI, mpk business yko itakapokuwa stable enough. Otherwise unaweza ukachukua mkopo na ukapotea, alafu na kazi uliyokuwa ushaacha so itakuwa ni mateso jasho na damu.
 
Daah...wenzako nssf inakimbilia mia, wewe sita una mind !?
 
eti anachukua mkopo kisha aache kazi...

kwa utawala huu wa magufuli nadhani utachukua nafasi ya babu seya...
 
Ndugu sikushauri uchukue mkopo afu ulale mbele huo ni wizi na hata biashara utakayoenda kufanya kufanikiwa kutoboa itakuwa ngumu sana kwako
 
Ndugu sikushauri uchukue mkopo afu ulale mbele huo ni wizi na hata biashara utakayoenda kufanya kufanikiwa kutoboa itakuwa ngumu sana kwako
umenena vyema mkuu

jamaa anadhani mungu kapotezea kama hamuoni.kumbe mungu anaona..

lazima upite njia ambazo mungu anaziridhia ili utoboe kimtindo
 
Ipo Taasisi ya Mikopo naifahamu ambayo dhamana ni ajira yako(Mtumishi wa umma), endapo kwa namna yoyote ile utakosa kuendelea na kazi, kuna insurance inayo-cover huo mkopo. (Mwajiri hayupo responsible kwa deni lako) Tatizo lao ni moja tu, kuwa makato yao yapo juu. Nadhani hii itakuwa njia muhimu kwako. Ukihitaji kuifahamu hiyo Taasisi nijulishe inbox nikutajie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…