Ushauri mpya kuhusu uvaaji wa Barakoa (Masks) kujikinga na maambukizi ya Covid-19: Tujielimishe ili tuamue vema

Haya, nimekubali graphs za kwanza zilikua hazileti interpretation uliomaanisha. Nimeweka hizo zinaonesha trends based on new cases. Je, zinawasilisha ulichokisema? Maana naona labda za S. Korea na Taiwan pekee ndio waweza kusema kuna consistent declining of the number of new cases.

But as said before, we have to know which cases are these. Je wanapima kila mtu kama wafanyavyo USA now au wanapima critical cases pekee kama wafanyavyo UK?

Pili, ni sahihi kutumia factors moja pekee kati ya nyingi wanazotumia na kusema ndio imeleta matokeo chanya?

Ninashawishika kwamba haya maswali yanahitaji tafakuri pana na data zaidi.
 
Hahahahaha

Wote waliokuwa wanapiga vita niqaab na hijab za Kiislam, sasa watafunika nyuso zao wakipenda wasipende.

Allahu Akbar.
kha.... mizigo mingine mnayojitwisha kwenye bongo zenu huwa inaharibu network kabisa..
 
Bandiko lako linadai hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa barakoa ni kinga dhidi ya maambukizi, lakini hapo hapo kuna ushahidi kwamba aliyeambukizwa akivaa barakoa anapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa yeye kuambukiza.

Kwa hoja hiyo, ni dhahiri uvaaji wa barakoa kwa watu wengi utapunguza wimbi la maambukizi.

Je, ni aina gani ya barakoa zitafaa?

Kwa hoja zilizo kwenye bandiko lako, barakoa yoyote itakayofunika mdomo na pua kuzuia makohozi na chafya zinazobeba virusi vya CORONA, itapunguza kusambaa.

Kwa kuwa hakuna anayejua kuwa ana maambukizi hadi apimwe, barakoa ivaliwe na kila mtu kama kinga mbadala ya kuzuia kusambaa kwa virusi na siyo kinga ya maambukizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…