Ushauri: Mtaji 26m Biashara ya Auto Parts, Lubricants & Spanners

Joined
Oct 25, 2021
Posts
98
Reaction score
98
Wakuu hii ni kuhusu biashara ya spares za magari, spanners na lubricants zote.

Ningependa kujua huo mtaji wa 26m utatosha nijizatiti vizuri?

Je maeneo gani yanafaa kuweka biashara ya aina hii ili nipate mzunguko mzuri?

Je hii ni idea nzuri au nitakuwa nimemwaga pesa ambapo sitapata return

Nasikilizia mawazo yenu
 
Wewe unautaalamu wowote wa ufundi garaji?
 
Bora kama umeamua kufanya hii biashara na kwa hela hiyo afadhali ujikite kwenye Lubricants tu na hela hiyo ni nzuri kwa kuanzia
Weka Oil za kila size na angalia ni aina gani zinatoka sana (fanya utafiti)
Hata kuzungukia garage utaona

Weka maji ya battery, brake fluid, Hydraulic oil
Hapo unajikita na hivyo tu kwanza ni rahisi kuhesabu hata kama unamuachia msaidizi
 
Mkuu nina experience ya miaka 2 ktk hii biashara, kiukweli ni nzuri,ila nakushauri tengeneza urafik na mafundi gerage

Wenye wagari wengi wakifika gerage wana waachia mafundi gari yaan ndio akague gari wapi bovu..

Sasa fundi ndio anakagua ugonjwa na huwa wana tabia ya kuongeza ata ugonjwa


Pia ukianza nakushauti uanze na spare za chin huko ndiko.magari.mengi huaribika e.g bush, cv joint, stablizer link, bearing, fan belt ... Brake pads na shuu zake,
 
Very nice, ahsante, mkuu
 
kwa ushauri wa kawaida idea n nzuri ila pata link up na watu wenye magarage hutojutia uwekezaji wako maana wale watakupa dairly and permanent consumption ya bidhaa zako na waweza pata vijana ukawa wawapa tips kwa kila kiwango cha manunuzi wanafanya kwko lazma wapeane mchongo kuvamia duka lako
 
Usifanye biashara kutegemea linkage ya magarage, hizo ni hopes zitakufilisi siku 1.

Wataanza kukopakopa kwako, wanasema boss hajatoa hela, kumbe ametoa wao wameificha. Utawapa mzigo, boss anakuja chukua gari yake na wewe unaanza kupigwa tarehe.

Atakuja kununua tena then atafuatia na mkopo. Baada ya muda utakuta una lundo la mikopo na hao magarage boys watahamia kwa mwingine. Akili ikikukaa sawa ushafilisika.

Kuna duka nalifahamu, kuna garage boys wamekopa wana hadi madeni ya 800k ya miaka mitatu nyuma tena huyo ni fundi mmoja tena ni dei waka. Na mafundi wengine wanaondoka wameacha madeni nyuma. Utaishia kuweka mtaji mpya kila siku kwa matumaini ya kulipwa madeni yako.

Usifanye biashara kwa kutegemea biashara ingine, wewe ndo unageuka target. Tena hizo biashara zingine ni informal kama hizo garages, utalia kilio kikuu.

Unless unafanya mutual relationship na well established institutions zenye each and everthing clear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…