Bank nyingi hazitoi mikopo ya ufugaji ila jaribu TIB kwenye dawati la Kilimo Kwanza. Majibu utakayopata tushirikishane kaka.
Nina shamba la ukubwa wa hekari 4 katika kijiji cha Vikawe karibu na Mapinga Bagamoyo ambalo nimelisajili kwa hekari mbili mbili (yaani lina hati mbili), ambalo nataka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji (lakini kwa njia za kisasa). Nahitaji mtaji wa si chini ya Tshs 15m ikijumuisha kuweka mabanda na uzio.
Swali: Je, ninaweza kutumia hati hizo za umiliki ardhi hiyo kama bond kuweza kupata mkopo benki kwa ajili ya mradi huo? Kama jibu ni ndio, basi ni benki ipi/zipi hizo?