Ushauri mzuri kwa wadogo zangu.

Ushauri mzuri kwa wadogo zangu.

Joined
May 23, 2024
Posts
15
Reaction score
43
MDOGO WANGU!

Dada yako Eva Mrema, nimewiwa kukuambukiza maarifa. Haya ni mambo matano ambayo nakuomba sana uyawekee mazingatio katika umri wa ujana kuelekea utu uzima wako.

1. ZINGATIA KUJIKUZA.
Katika umri wa ujana mbichi binti wa kisasa unawaza usome, uhitimu; upate kazi, upate mwanaume mwema na mwisho uwe na familia unayoiota. Chochote unachofanya wakati huu, unazingatia zaidi kile unahisi watu wanataka kukiona kwako ili wavutiwe na wewe. Sio kosa, ni umri wa kufikiria hayo. Lazima upite kwenye safari ya kuwaza ukivaa nini utateka umakini wa kijana fulani unayehisi anajaa kwenye malengo yako. Lazima ujipimie chakula na muda mwingine ule usivyovipenda ili mwili wako usiharibike. Lazima utembee na kujali kila mja anavyokutazama. Ngoja nikwambie! Wengi tunafanya hivyo. Binafsi sikutambua mapema kwamba mitazamo ya watu daima ni yao na haiwezi kunipa mimi furaha. Sikujua kabisa kwamba nilihitaji kuwekeza muda kwenye ukuaji wangu wa moyo na akili. Sikufikiria hata robo hisia zangu. Nilitaka tu kuwa kama mabinti wengine wawavyo wafikiapo umri fulani. Kumbe basi, nilitakiwa kujikuza, kujichochea na kujizingatia katika yote mema. Tabia, mienendo sambamba na mihemko yangu ilinihitaji mimi mwenye maarifa ya kuiboresha. Hivyo jiruhusu KUKUA, ishi kwa kufuata sheria taratibu na tamaduni za mazingira uliyopo lakini heshimu sana hisia zako. Unahitaji furaha, unahitaji kujisikia vizuri katika maisha yako na kazi hiyo ni yakwako wewe.

2. USIRUHUSU HOFU YAKO IKUZUIE.
Asiye na hadithi ya kuanguka maishani ni yule ambaye hajawahi kuwepo. Wakati mwingine tunaanguka vizuri baada ya kuhofia kuanza upya baada ya anguko dogo la kwanza.
Hofu iko hapo kutuua kama tutashindwa kuiua. Usiruhusu hofu yako kukuzuia kuanza upya. Hatua yako mpya ya kwanza baada ya kumpiga bwana hofu ni hatua yako ya kwanza kuyaendea mabadiliko unayotamani yatokee kwako. Haumuhitaji yoyote kuikimbiza hofu, unajihitaji wewe mwenye malengo na ndoto zilizo hai. Amka, iue hiyo hofu, haitakiwi kuwa na udhibiti juu yako, safari ni ndefu mdogoangu.

3. MARAFIKI.
Jaribu kuwa na marafiki walioko tofauti na wewe. Ni ngumu na wakati mwingine ni changamoto sana ila ugali unaliwaje na ugali kama mboga? Ni hivi, hasi na hasi hakuna matokeo mazuri wala mabaya. Si vibaya kuwa na rafiki wa shida na raha lakini jiconect na watu walio tofauti na wewe. Yaani hakikisha kwenye mzunguko wako kuna watu ambao wanakupa wivu wa maendeleo, wanakusukuma kuongeza elimu, wanakushauri kuhusu mahusiano na maisha kwa ujumla. Nimebadilika mengi baada ya kubadilisha mzunguko. Fikiria tu, wewe ni single girl uliyeumizwa na ma play boy.. marafiki zako nao ni kama wewe tu, nani atamwambia mwenzake juu ya uwepo wa watu wema wa jinsia nyingine? Ni nani atamwambia mwenzake arudi shule ikiwa nyote ni lasaba B? Tunachochewa na shuhuda malengo yakisinzia. Tunahitaji watu ambao wako ngazi tofauti ya maisha, ama chini au juu, kuna mabadiliko kwenye utofauti.

4. JITUMBUKIZE KWENYE JAMII.
Ngoja nikupe kakisa kidogo kunihusu. Napenda sana kusafiri na kwenda sehemu nisizozijua. Nilisafiri mwaka fulani na kwenda Tabora. Sikuwa na mwenyeji na sikuwa najua chochote kuhusu mji ule wenye watu wakarimu. Nilijitumbukiza mtaani. Nilitengeneza ndugu na marafiki, kiufupi ilibaki nukta nipewe mume 😄. Nilitoka jiji la mbali na kibunda changu kujipa tu uzoefu wa maisha tofauti, kama ningejifungia hotelini nilipofikia ni lini ningekula matobolwa? Ni lini ningejua Tanzania ina watu wema namna ile? Ni hivi, wakati wa ujana mbivu, yaani 22-27 ni wakati wa kupata uzoefu wa maisha nje ya unayoyajua. Jitimbukize kwenye jamii, husiana na watu hata usio wajua. CONECT, kuna vitu watu wamezeeka wanafanya vya aibu kwa sababu tu waliruka vipengele wakati wakiwa na uhuru wa kimazingira. Safiri, sio lazima uende kwenye vivutio. Sio lazima uende kwenye miji mikubwa, kama unaweza toka wilaya moja nenda nyingine, kaa siku mbili, jichanganye, shirikiana na hiyo jamii, tengeneza wana wapya kisha rudi.. kuna uzoefu wa kipekee sana utaupata kwa kufanya hivyo.

5. UTAKUTANA NA MAKWAZO TU.
Mpendwa!
Ukweli mchungu wenye ladha ni kwamba makwazo hayana kinga. Utakutana na wakatisha tamaa.
Utakutana na wanyonyaji.
Utakutana na wafitini pamoja na waua ndoto. Utakutana na wale jamaa wa changu changu chako ni chetu.
Utakutana na wanafki, waongo pia wababaishaji.
Utafanya mambo yataenda tofauti.
Utapanga mipango kwa akili, itabuma.
Utalima, utapalilia utaweka mbolea kwa usahihi ila mvua zitanyesha nyingi na kuozesha mazao.
Utatapeliwa na mengi yafananayo na hayo. Kiufupi, utakutana na makwazo ya kila aina. Utakutana na mambo usiyo yatarajia naomba uweke tu akilini neno hili MAISHA HUANZA KULETA MAANA BAADA YA KUVUKA MAKWAZO..

PIA....
Usichoke kujifunza.
Acha kufikiria kila kitu ni kuhusu wewe.
Acha kujishuku.
Sio mara zote utakuwa na mipango, kubali kupumzika.
Ni sawa kubadili mitazamo kila inapobidi.
Jitahidi kusoma maandiko ya kukujenga.
Fanya ibada.
Mungu akusaidie.

©️ ✍ Malkia wa tabasamu
kungwi wa kisasa.
 
Nzuri, Asante.
 
Back
Top Bottom