Voice of Wisdom
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 537
- 240
wadau wa ujasiriamali poleni kwa majukumu ya kujenga uchumi wenu na taifa bila kusahau mafisadi.
Nimechukua hatua ya kuandika uzi huu baada ya kuona jambo hili linajirudia mara kwa mara na watu pengine hawajagundua kuwa ni TATIZO.
Nimekutana na post nyingi karibu kila mwezi post mpya yenye kichwa NINA MTAJI WA TSH .... NISHAURINI NIFANYE BIASHARA/KITU GANI?
Kiukweli hili swali si swali la kuulizwa na mjasiriamali.
Kwa nini?
Kwa sababu mjasiriamali yeyote mtaji si fursa ila wazo la nini cha kufanya ndiyo deal. Katika ujasiriamali watu hawaanzi kutafuta mtaji kwanza wanaanza na wazo la biashara yenyewe:
je ni biashara ya aina gani?
Soko lake likoje?
Upatikanaji wa bidhaa
washindani walioko sokoni (uwezo na udhaifu wao)
Jinsi ya kufika sokoni(miundombinu)
Sheria zikoje?
Mtaji utakaouhtaji? n.k
Mjasiriamali makini lazima afanye upembuzi wa biashara yake (business feasibility analysis).
Na katika upembuzi huo mtaji ni end product, mtaji si fursa, mtaji ni matokeo ya fursa uliyoiona na kuifanyia upembuzi. Tafuta fursa ndiposa utafute mtaji kulingana na fursa yenyewe.
Haihitaji elimu ya ujasiriamali kuona fursa ila moyo wa ujasiriamali.
Ujasiriamali huanzi na mtaji bali wazo la biashara
"NA HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU"