Ushauri na Mawazo yenu Muhimu!

DALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
2,256
Reaction score
4,647
Heshima mbele wakuu!

Nakuja kwenu kuomba ushauri ili niweze kufanya maamuzi yenye tija katika kuendeleza ujasiriamali wangu.

Iko hivi, mimi ninafanya biashara mbali mbali kwa kiwango changu sasa miaka minne iliyopita niliamua kuwekeza katika biashar ya kuosha magari. Nikapata sehemu hapa mjini tukakubaliana na wazee wenye eneo ambapo nilitekeleza yale yote niliyotakiwa kufanya ili nipatumie pale ikiwa ni pamoja na kuwajengea choo na bafu ya kisasa kwani pale ambapo nimejenga car wash palikuwa na choo (passport size).

Kwa kweli kutokana na ufinyu wa nafasi nilitumia gharama kubwa sana kuwajengea hata na bonge la chemba underground ili ku maximize matumizi ya eneo lile.

Nilipomaliza ujenze na kufanya process ya application ya umeme Tanesco ambayo ilichukua muda kidogo nililazimika kuomba umeme kwa jirani ili nianze kazi mdogo mdogo mpaka pale nitakapounganishiwa umeme.

Tatizo likaanza sasa na wazee wangu wenye nyumba. Kwanza tulikubaliana kwamba mpaka pale Tanesco watakapo niunganishia umeme ndo tutaamza kazi rasmi na kuanza kuhesabiana kodi maana niliwalia hela hata kabla ya kuanza ujenzi kodi ya mwaka mzima. Wazee walinigeuka na kusem hela niliolipa siyo kodi ya pango bali ni ya ujenzi, pili wakataka kunipandishia kodi mara nne ya kiasi tulichokubaliana mwanzoni baana ya kuona pale pameng'aa. Aisee tulibishanaaaaaaa. Lengo lao ni kwamba kwa kupandisha kodi, wataweza kunirejeshea invested capital ndani ya mwaka mmoja alafu wanitimue.

Mungu mwema niliweza kukataa nikashangaa naitwa serikali ya mtaa. Tulipofika kula baraza la serikali ya mtaa wakaona ule mchezo ya wazee ikabidi wanisaidie nikapata mkataba wa miaka saba pale. Nikamshukuru Mungu maana walidhamiria kunjdhulumu.

Sasa mwaka mmoja na nusu baada ya pale wamerudi kwa njia nyingine kwamba wanataka kusitisha mkataba. Nilishangaa napigiwa simu kutoka serikali ya mtaa kwamba wazee wana hela zao wamempata mwekezaji mwingine wanataka kunirudishia hela yangu. Mimi nilikataa maana mkataba wa miaka saba siyo ndogo hivyo nikawaambia wapige mahesabu ya ninachokipata pale kwa mwezi mara miaka iliyobaki ile mitano. Wakagoma nami nikagoma.

Kesi ikapelekwa baraza la kata, tulipofika pale kwanza sikuridhika na integrity ya katibu na baraza zima kwani wao walichohitaji ni gharama ya kusikiliza kesi na hawakufanya uchunguzi kuelewa kesi na madai vizuri ila hatimaye nilishangaa kusikia nimepiteza kesi hivyo nitalipwa hela ambao wao ndo waliamua. Ni ndogo sana ila baada ya kushauriana na watu ikaonekana niepushe shari maana wale wazee ni wa uswahilini, ushirikina wananitishia kila siku basi bora nichukue hicho kiwango nihesabu hasara. Nikakubali kupokea zile pesa ila bahati mbaya kwao ni kwamba siku ninatoa maelezo kwenye baraza la kata walimleta yule aliyetaka kunirithi biashara so yule jamaa alisoma mchezo wa wazee badae akaingia mitini.

Baraza limeamua wanilipe na nisiendelee na biashara pale tarehe ikapangwa ya wao kunilila naona kimya. Kufuatilia wanasema wao hawana hela na yule aliyetaka kupachukua pale toka siku tulipokutana kwenye baraza la kata hajaonekana.

Nikaona isiwe tabu, nikaenda kwa wakili anisiaidie nipate kile kilichochangu kwa wakati, mahakamani hiyo tena, wito ikapelekwa sasa hawana hela, na kwa muonekano nyumba yao itapigwa mnada. Kwa sasa wao wananionea aibu wameamua kumtumia mtoto wao mmoja aliyeko Singida anishawishi nirudi kufanya biashara pale na nisamehe yote wakati mimi hata vifaa vyangu baadhi nimeshauza maana ofisi niliamua kufunga kabisa.

Wakuu, kwa historia ndefu hii mnanishauri ninj?

Mbarikiwe sana
 
Mhhhh! Pole sana, kuingia mkataba na watu wasiothamini mkataba na waliojaa tamaa ya pesa ni hatari sana. Kama unaweza kuvinunua hivyo vifaa ulivyoviuza fanya hivyo ili uweze kuendelea na biashara yako. Vinginevyo itakula kwako maana hao wazee "hawana pesa" za kukurudishia.
 

Tatizo ni kwamba siwaamini tena alafu wana maneno ambayo mwenyewe utakimbia
 
polee mkuu.wazee wakiuswazi ni shiiidaa.
 
Ahsante mkuu. Wamenisababishia hasara ila naona mwendo ni ya kupiga nyumba yao bei kwa amri ya mahakama inakaribia
 
Ahsante mkuu. Wamenisababishia hasara ila naona mwendo ni ya kupiga nyumba yao bei kwa amri ya mahakama inakaribia
Mkuu pole sana, tamaa ya pesa bila kuwa na mipango ni sheeeeda. wazee walishawishiwa tu hao. kama waweza tafuta wazee wengine wenye busara na waeleze hali halisi, alafu mkae na hao wazee wenye hiyo plot. Ni kweli hawaaminiki lakini lakini kwa mbwembwe la mnada wa nyumba watafyata mkia.mtakachofikia mshirikishe na wakili na mkataba mwingine juu.alafu endelea kuchapa kazi wameshajifunza hao. pole sana mkuu.
 

Ahsante sana kwa ushauri mkuu. Nitajitahidi kufanya litakalo kuwa na manufaa ila ukumbuke waswahili kwa ushirikina pia ni sehemu ya maisha yao so kazi inakuwa ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…