Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kuliko mabinti, wasichana na wananawake pekee kujaza makanisa na masinagogi wakitafuta wenza na wachumba kwa maombi na maombezi kwenye nyumba za ibada,
Uko umuhimu wa kufanya kongamano la kitaifa na mikesha maalumu kwa vijana wa miaka 18-40, wa kike na kiume, ambao bado hawajaoa wala kuolewa, ili kuwapa mwangaza na maono ya kinabii ya namna ya kukutana na wachumba zao, pamoja na watu ambao Mungu amekusudia kuwaunganisha nao ili hatimae waishi kama familia takatifu kwa ndoa.
Kwanza wawakutanishe vijana wa kiume peke yao na kuwafunda namna ya kiMungu na ya baraka jinsi ya kumtambua na kupata mwenza wa kuishi nae katika maisha ya ndoa yenye upendo, furaha na amani. Halafu tena wakutane na vijana wa kike nao vilevile wafundwe vyema namna ya kutambua mume mwema na jinsi ya kuishi kwa furaha katika ndoa yao na watoto wao Mungu akiwafanikisha.
Halafu sasa, baadae lifanyike,
kongamano na mkesha maalumu wa pamoja, kwa vijana wote wa kike na kiume, na tahmini ya mafanikio na matokeo ya makongamano na mikesha hiyo ifanyike mwisho wa mwaka, kwa ndoa maalumu takatifu za makundi ya pamoja kwa ambao Mungu atakua amewaunganisha kupitia mikesha na makongamano hayo maalumu ya kiroho.
Napendekeza maombi na maombezi ya kinabii namna hii yawe yanafanyika kila mwanzo wa mwaka, na kisha tathmini ya matokeo yake vifanyike katikati na mwisho wa mwaka kwa ndoa takatifu za makundi ya pamoja kufanyika.
Hii hali ya kujaza wanawake na wasichana pekee makanisani itakua na maana tu, endapo patakuwepo na kampeni maalumu ya kiroho na kinabii, kuhakikisha na vijana wa kiume pia wanajaza makanisa. Kwa kufanya hivi, manabii na mitume watakua wamesaidia sana hii kasumba ya kutangatanga miongoni mwa vijana wasio oa wala kuolewa kwenye makanisa mabalimbali ya kiroho.
Neema, Baraka na Upendo wa Yesu Kristo wa Nazareth viwe nanyi nyote, sasa, daima na milele, Aimen.