Ushauri na wosia wangu kwa Wakuu wa Wilaya walioteuliwa na Rais Samia

Ushauri na wosia wangu kwa Wakuu wa Wilaya walioteuliwa na Rais Samia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Kwanza napenda kuwapa hongera, hongereni sana kwa wote mlioteuliwa kuwa maDC nendeni mkachape kazi.

Wote mlioteuliwa mimi nawafahamu vizuri ni vijana mnaojituma sana kwenye jamii. Jamii inawafahamu jinsi mnavyotumia akili na uwezo wenu kwa weledi katika utafutaji na ujasiliamali mbalimbali.

Leo sitakua na mengi sana, ila nawasisitiza sana sana kachapeni kazi.

Rais amewaamini na sisi tumewaamini kawatumikieni wanainchi.

Kazi ya u-DC ni kazi ya kuwatumikia wanainchi.

Kahakikisheni kwenye wilaya zenu maji yanapatikana, umeme unapatikana, kahakikisheni shule zinapatikana, kahakikisheni watoto wanakalia madawati shuleni, kahakikisheni watoto hawakai chini, kahakikisheni barabara zinapitika katika wilaya zenu, kahakikisheni kwenye wilaya zenu kuna umeme wa uhakika, kahakikisheni kwenye wilaya zenu ulinzi na usalama unaimalika.

Mkajiongeze kwenye wilaya zenu kuna rasilimali mbalimbali kuweni wajanja kama sungura vutieni wawekezaji. Ukiwa mzubaifu huwezi kuleta wawekezaji.

Kwenye wilaya zenu kuna vivutio vya utalii nendeni mkavitangaze ili vijulikane.

Mkahakikishe hakutokei ubadhilifu wowote wa fedha zetu za Miradi.

Mkahimize wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo kwenye wilaya. Wilaya ni kitovu cha maendeleo ya mkoa.

Mkuu wa wilaya kama mwenyekiti wa timu nzima ya viongozi wa wilaya kahakikishe unaimarisha mawasiliano mazuri na ushirikiano kwa viongozi na watumishi wote wa timu yako ili kuleta ufaninisi mzuri wa shughuli zote katika wilaya yako.

Kama unahitaji ushauri zaidi njoo inbox nitakushauri. Ofisi yangu ipo wazi muda wotewote.
 
Ukweli ni kwamba wanaenda kuhakikisha kwa namna yeyote ile CCM inashinda 2025 kwa kishindo pamoja na kuangalia maslahi yao binafsi.

Wote tulikuwepo tumeona yaliyotokea tangu 2005 mpaka sasa kwenye hivyo vyeo.
 
Back
Top Bottom