MWALIM WA KIJIJINI
Member
- Aug 22, 2013
- 66
- 66
ndo nini hiyo speak!!gari gani ambayo spea zinaagizwa Nairobi!Toyota ndio magari yanayoongoza kwa speak kupatikana kirahisi, na hilo ndio muhimu. Jihadhari usije nunua gari ambao spea inabidi uziagize Nairobi.
Vv
Too much of any thing is harmfulAudi uwe tofauti ist baby walker
ndo nini hiyo speak!!gari gani ambayo spea zinaagizwa Nairobi!
Kwa Tanzania magari Aina ya Toyota ndiyo prefence, kwani spare zake ni nyingi kuliko gari aina yoyote zinazo onekana hapa.
Kama unahofia mafuta bora ununue pikipiki,1ltr unaenda hadi 25km,Mnunuaji wa gari aangalii ulaji wa mafuta,kama umeweza ku-make hadi kufikia uamuzi wa kununua gari ya thamni zaidi ya 10m utashindwaje mafuta?
fuel economy ni muhimu kwa mtu wa kipato cha kawaida, usije jikuta gari inatafuna mafuta ya elfu50 kila siku wakati mshahara wako 1.5M kwa mwezi, utaanza kutembea kwa miguu kila ukikutana na jirani unaanza kujishauwa uko kwenye kampeni ya kupambana na kitambi wakati mtu mwenyewe uko safi hauna kitambi. Ukiona mtu anaingia petrol station na kujaza mafuta ya elfu6 ujue hiyo gari inambaka vibaya mno, akikuta watoto wa jirani wanasubiri daladala kwenda shuleni anawachunia wakati wanasoma shule moja na wake. Wengi hatujuwi kujipimia kulingana na uwezo, mtu anajikamua kununua Crown Majesta wakati safari yenyewe mara moja kwa mwaka, tena haendi zaidi ya morogoro, anataka kuwaonesha walimwengu tu kuwa ana gari "kali"..gari kali inakuwaga mtumba!? Kinachofuata hapo ndani ya nyumba anakuwa mkali tu, mama akisema anataka kwenda sokoni anazua visingizio, watoto kuwapeleka sehem anasema mko wengi pandeni daladala....anawaza mafuta tu!
Du kama ndio hivyo basi bora asinunue gari,ya nini ninunue gari ya cc 500 nikipitiwa na lori tu napepesuka kisa ni fuel economy? For me nah no go so........
lipitwe na roli ukienda wapi, jangwani kufundisha twisheni?...lol
Kwanza jiulize unahela ya kununua gari?,bila shaka unayo ndo maana ukasema,pili jiulize unahela ya kulimudu gari kiuendeshaji?,isije fika mahala ukaanza hadi kutumia hela ya mambo muhimu ktk kufanya gari liwe barabarani,watoto wasije punguziwa matumizi ili tu gari liwe barabarani,naamini uko makini na halitatokea hili,t
Tatu,una hitaji gari kwa matumizi gani?,isijekuwa ni mkurupuo tu wa kutaka kuwa na gari,tambua kwanza matumizi unayotaka kufanya nanhilo gari ndoujiulize utanunua gai gani kulingana nanmatumizi,km ni la biashara tafuta gari linaloendana na aina ya biashara,
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kukuongoza na kujiuliza kabla ya kununua gari,kitendo cha ww kuuliza tu humu ni ushahidi tosha kuwa ww ni mgeni na magari hvo nnaloshauri usikurupuke,haya magari yanamatatizo zaidi ya tunavoyaona watu wakimiliki,km si muda sahihi usinunue,na km ni muda sahihi tafuta gari sahihi kulingana na unachotaka kulifanyia,epuka magari ya mikononi na midomoni mwa watu