Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Boss Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
458
Reaction score
991
Wakuu nimerudi tena, Nadhani mtakuwa mnaniona hapa mara kwa mara Kila nitakapopata changamoto

Juzi kati nilipata safari ya Dodoma nikaenda na Beamer (BMW X3) na ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza naenda safari ndefu na hii gari

Wakati naenda muda wa kulifanyia service ulikuwa Bado haujafika zilibaki kama kilometers 1,200 plus nikaenda Dom nikarudi zikabaki kama kilometers 200+ ili zitimie kilometers 3,000 muda wa kufanya service ufike

Sasa Wakati narudi nilivyofika mbezi Taa ya Engine oil ikaniwakia (yellow) nikafika nyumbani, jana nikalipeleka Mikocheni kwa lengo la kuongezwa oil

Mikocheni Coca-cola Garage ya Atlantic lakini nilivyofika jamaa wakanambia kabla ya kuongeza oil itabidi walicheki kwanza kama kuna leakage wakacheki hawajakuta leakage yoyote ila wakanambia itabidi walifanyie Service kabisa maana oil wameikuta ni nzito tofauti na inavyotakiwa (nikakubali)

Waka change Oil na Oil filter Gari ikakaa sawa, nikapewa invoice total ikaja Tsh 483,800,

Ile Quotation Iko hivi

Oil 8 liters 350,000
Filter 60,000

Subtotal = 410,000/=

Vat 18% 73,800

Total = 483,000/=

Swali langu ni kwamba ukilifanyia Gari service na haina leakage yoyote Oil inatoboa hadi next Service au hapa katikati inabidi uiongezee?

Na je kwa situation yangu ya jana ni kweli ilibidi gari lifanyiwe Service au walivutia upande wao wa kibiashara, Wajuzi naombeni mshee experience zenu
 
Kwanza unatakiw ujue OIL kupungua sio tu kuwe na leakage, heat pia inachangia OIL kupungua.

Sion shida kama muda ulikaribia wa kufanya service na ww ukafanya service. Pia unachotakiwa kuwa nacho makini ni hivi.
Oil iliyowekwa ni recommend na Manufacturer?
Je Oil filter ni sahihi?
Je after kufanya Service umepewa Service breakdown na estimated Kilometers za kutembea..?

Pia jitahidi kufanya follow up kila siku kabla ya kuwasha gari.

Ni hayo
 
kama gari haina leakage yoyote inatoboa hadi service nyingine na mara nyingi inategemea na oil unayotumia kwenye gari lako zipo oil hadi 5000km ndo unabadili. Ikitokea gari lako oil inapungua ujue kuna shida kwenye gari lako mana gari lenye mfumo mzuri uwezi ongeza oil ni service hadi service.
 
amenifurahisha hapo alitaka ongeza oil baada ya kuona zimebaki 200km [emoji28][emoji28][emoji28]
Kwanza nimeshangaa anabadili oil kwa 3k km. Hv pale kwenye mfuniko si wamesema castor oil kabisa na mzigo ni km 10k ukichelewa na gari kwanza yenyewe itakuambia service now[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2925]
 
Wameniambia nikuulize kabla hawajaanza kuja, ilo Beamer ni lako au la shemeji yako 💃
Beamer ni BMW Motorcycle
Bimmer ni BMW car..!

Kama oil ilipungua na muda wa service umekaribia sana 200km..then option waliyoifanya ni nzuri.. Kucheki leakage na kubadilisha yote..!
Inawezekana kwenye safari gari ilikimbia sana ikachoma oil ndio maana imepungua..!

Kama itaweza kutoboa next service utapata majibu kwenye dashboard..!
 
Kufanya follow up kivipi mkuu, nifafanulie, kuhusu Kilometers ni Kila baada ya kilometers 3,000
 
Kufanya follow up kivipi mkuu, nifafanulie, kuhusu Kilometers ni Kila baada ya kilometers 3,000
Kanuni za Udereva hutakiw KUWASHA gari bila kufanya UKAGUZI.

Ukaguzi upo wa ndani na upo wa nje

Ukaguzi wa Ndani unahusu Gari kwa ujumla mpk Injini. Hapo ndio utapima na Oil kulingana na Deep stick ya oil, maji (Coolant) hydraulic mpk brake fluid.. etc.

Ukaguzi wa Nje ni ENVIRONMENTAL based, unaangalia Uvunguni.. Nyuma au mbele ya matairi kuna sharp objects? Je kuna Mtoto au Mnyama Kalala?

Hiyo ndio maana ya daily follow up
 
Tuongee uhalisia kidogo, wewe unafanya haya Kila siku?

Kwa upande wangu mimi sifanyi hayo kila siku kutokana na mazingira yenyewe hasa hiyo ya kulala chini sijui kuangalia chini, na kuhusu vitu vingine Gari inanionesha Kila Kitu kwenye Dashboard Sasa Kuna haja gani ya kufungua Bonnet
 
Ndio maana mnaua Magari bila kujijua. Gari zinawaka Moto kwa makosa madogo tu unawz kuta Bonnet cover imesogea au imeachia je utajua ktk Dashboard? Je deep stick imepanda juu na kuruhus Oil kuvuja na kufata exhaust pipe utajua? Unajua madhara yake?.. Gari kila siku ikague na kama muda upo Pima/hakikisha bolt za matairi zimekazwa vzr at least kila baada ya wiki unafanya Uhakiki
 

Hiki unachosema ni vizuri ila nakubaliana na jamaa mtoa mada kwamba inawezekana hata wewe hufanyi hivyo kila siku (au niseme watu wengi hatufanyi hivyo kila siku kuhalisia). Ndio maana warning kights kwenye magari ya kisasa ji nyingi, ikiwaka unakagua.
Kama mna uzoefu ma hizi gari mshaurini tu frequency ya kufanya service, oil type etc. uzuri gari nyingi za Ilaya zikiwa na shida unapewa kila kitu kwenye dash. Binafsi naona kama kauziwa oil bei ghali sana. Na oil recommended inatakiwa kutoboa KM 5000. Ikibaki km chini ya 500 sio mbaya unaweza bado kufanya service tu kwa sababu ni rahisi kumaliza huo umbali na ukawa sehemu usiyoweza kufanya service.
Lakini pia nakubaliana kiujumla na wazo la kujenga tabia ya kukagua gari from time to time
 
Yaah ,mie Binafs nimeanzia kuendesha Gari mbovu ( Lazima Uweke Maji asubuhi au baada ya muda) nje ya hapo Unakaanga Gari so Mazoea hujenga tabia, Kukagua ni Tabia yangu maana madhara yake ni makubwa usipo fanya hivyo iwe gari ya Zaman iwe gari ya Kisasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…